Connect with us

General News

Wingi wa washindani wa ugavana Vihiga wavurugia ANC hesabu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wingi wa washindani wa ugavana Vihiga wavurugia ANC hesabu – Taifa Leo

Wingi wa washindani wa ugavana Vihiga wavurugia ANC hesabu

NA DERICK LUVEGA

JUHUDI za chama cha Musalia Mudavadi, ANC, kunyakua kiti cha ugavana katika Kaunti ya Vihiga kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa ugatuzi zimegonga mwamba, baada ya kutokea mgawanyiko kati ya wapigakura wa jamii ya Maragoli.

Mgombeaji wa kiti cha ugavana na rafiki wa karibu wa Bw Mudavadi, Bw Alfred Agoi ameeleza kuwa kujitosa kwa wagombeaji wawili wakuu kutoka kwenye makabila mawili yenye wapigakura wengi zaidi katika kivumbi hicho, kunazuia ANC kufikia ndoto hiyo bila pingamizi.

Vihiga ni ngome ya Bw Mudavadi na chama chake kinanuia kushinda kiti hicho ambacho mwanzo kilikaliwa na Bw Moses Akaranga wa chama cha PPK na sasa Dkt Wilber Otichilo wa ODM.

Muungano wa Kenya Kwanza ungefaidika iwapo Bw Akaranga hangejitosa ulingoni kuwania kiti hicho.

Kulingana na wadadisi wa kisiasa, Bw Otichilo anaongoza kwa umaarufu na asilimia 33, akifuatiwa na Bw Agoi asilimia 31 na Bw akaranga kwa asilimia 20.

Kinyang’anyiro hicho kimekuwa na ushindani mkali baada ya Seneta George Khaniri, spika wa zamani Bw Kenneth Marende na Bw Francis Ominde (katibu wa Kaunti) kujitosa ulingoni.

Bw Agoi alitaka wapigakura kutoka jamii ya Maragoli, yenye wapigakura wengi zaidi, kumpigia kura na kuhakikishia ANC ushindi.

Pia alimwomba Bw Akaranga ajiondoe kwenye mbio hizo na kumuunga mkono.

“Makadirio yanaonyesha mimi ni wa pili kwa umaarufu hapa Maragoli. Shida ni iwapo Bw Akaranga atakuwa kwenye kinyang’anyiro hiki, kuna uwezekano wa kura za Wamaragoli kugawanyika. Bw Akaranga aniunge tu mkono kwa sababu alishakalia kiti hiki,” alisema Bw Agoi.

Bw Agoi na Akaranga wanatoka katika kabila dogo linaloishi Vihiga, Sabatia na Hamisi Magharibi.

Bw Marende anatoka eneo la Bunyore, ambalo ni la pili kwa wingi wa wapigakura., katika kaunti hiyo. Bw Khaniri naye anatoka kwenye kata ndogo ya Hamisi.

Haya yamejiri huku makundi ya viongozi wa kidini, wazee, wafanyabiashara na wataalamu wakimpendekeza Bw Agoi kuwa gavana mpya wa kaunti ya Vihiga.

Kupitia kongamano la Vihiga Consultative Development Forum (VCDF), waliwataka wagombeaji wote akiwemo Bw Otichilo kuacha azma zao na kumuunga mkono Bw Agoi wakimtaja kama kiongozi bora kwa maendeleo ya kaunti hiyo.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending