Connect with us

General News

Wito raia wavae maski wakisafiri – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wito raia wavae maski wakisafiri – Taifa Leo

Wito raia wavae maski wakisafiri

NA ELIZABETH MERAB

WIZARA ya Afya imeagiza Wakenya wote wanaosafiri katika magari ya umma, ndege na gari moshi waendelee kuvaa barakoa.

Wizara hiyo pia imesema watu wanaohudhuria mikutano ya ndani ukumbini pia wavae barakoa.

Wiki jana, wizara ililegeza baadhi ya kanuni za kudhibiti msambao wa virusi vya corona kutokana na kupungua kwa idadi ya maambukizi.

Serikali iliruhusu watu wavae barakoa kwa hiari yao.

Hata hivyo, akitangaza afueni hiyo wiki jana Waziri wa Afya, Bw Mutahi Kagwe, alisema wasafiri wote lazima wavae maski.

“Sharti la kuvaa barakoa katika maeneo ya umaa limeondolewa.

Hata hivyo, Wakenya wote wanafaa kuvaa barakoa wakiwa katika hafla za mikutano za ndani na wakisafi – ri,” ikasoma sehemu ya ripoti ya wizara hiyo.

Janga la corona lilipolipuka ulimwenguni, kila nchi ilibuni kanuni zake za kuthibiti msambao wa virusi hivyo. Baadhi zikiwa sharti la kuvaa barakoa na kuweka kafyu.

Hata hivyo, katika miezi iliyopita mataifa yameendelea kulegeza kanuni hizo kuambatana na jinsi maambukizi yanazidi kupungua.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending