– Sarah amesema aliacha vileo kwake na huenda vikaharibika na hivyo kuitaka mahakama kumpa ruhusa kufika huko
– Anateta DCI walichukua umiliki wa nyumbani kwake na hivyo hawezi kupata mali yake
– Mshukiwa huyo anatuhumiwa kuwa mmoja wa waliomuua mumewe Tob Cohen
Mshukiwa wa mauaji ya bwenyenye Tob Cohen, Sarah Wairimu Cohen, amefika mahakamani akitaka apate ruhusa ya kufika kwa nyumba yao kwenye mtaa wa kifahari wa Kitsuru.
Sarah, ambaye alikuwa ni mkewe Cohen, aliambia mahakama Jumatano, Novemba 13, kuwa anahitaji kufika kwake nyumbani ili kuchukua baadhi ya bidhaa ambazo anahitaji.
Habari Nyingine: Pasta Lucy Natasha awafurahisha wafuasi wake, apepeta mpira kwa ustadi mbele ya Musa Otieno
Mshukiwa wa mauaji Sarah Cohen aomba mahakama aruhusiwe kufika nyumbani kwake kuchukua mvinyo. Picha: Sarah Cohen
Source: UGC
Alisema aruhusiwe afike humo na kuwachukua mbwa wake wawili, vinywaji alivyowacha jikoni na kwenye afisi yake, vikiwemo vileo, nguo, mafuta, vyombo vya kupikia, bidhaa za kieletroniki, nguo, viatu baadhi ya vitu vingine.
Mshukiwa huyo alisema huenda vileo vikaharibika iwapo ataendelea kukosa kuruhusiwa kufika kwake nyumbani.
Kupitia kwa wakili wake Philip Murgo, Sarah anataka mahakama iagize mkuu wa DCI George Kinoti kuwachilia gari lake kwani maisha ya kutegemea magari ya watu anasema yamekuwa ghali mno.
Habari Nyingine: Janga la soka nchini: Harambee Stars karibu kufukuzwa hotelini Misri
Sarah Cohen aliambia mahakama anaendelea kuteseka licha ya kuwa ana bidhaa zake kwenye nyumba yao. Picha: Lemiso Sato
Source: Facebook
Mshukiwa huyo alikamatwa baada ya wachunguzi kusema kulikuwa na ushahidi kuwa alihusika katika mauaji ya mumewe.
Baada ya kukamatwa, mwili wa mumewe ulipatikana kwenye tanki la ardhini nyumbani kwao.
DCI walisema mshukiwa wa pili kwenye mauaji hayo Peter Karanja ndiye alisaidia mwili huo kupatikana.
Habari Nyingine: Ida Odinga, mkaza mwana Lwam wapewa wiki mbili kukubaliana
Sarah Cohen na aliyekuwa mumewe Tob Cohen. Picha: Nation
Source: UGC
Wawili hao wanakabiliwa na mashtaka ya mauaji na mahakama ilipomwachilia Wairimu kwa bondi ilimtaka kutofika kwenye nyumba yao ambapo kwa sasa ni maeneo ya uhalifu kulingana na DCI.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videos