Hata hivyo, kulingana na sehemu ya wadadisi, mpango huo umechochewa na uchaguzi mkuu ambao unatazamiwa kuandaliwa nchini humo mwakani, kama ilivyoripoti BBC.
Haya yanakujia siku chache baada ya Rais wa taifa hilo Yoweri Museveni kutaja taasisi zote za masomo kama nyasi kavu mbele ya moto wa janga la virusi vya corona na kusisitiza suluhu pekee ya masomo kwa sasa ni teknolojia.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema suluhu ya sasa ya masomo ni kupitia teknolojia. Picha: Yoweri Museveni. Source: Facebook
Museveni pia aliongeza kuwa masomo ya mbali huenda ndio bora zaidi kwani wanafunzi wengi watafaidika nao walimu wachache wanaweza kuwafikia wanafunzi wengi kupitia redio na televisheni.
Shughuli za masomo nchini humo zilisitishwa karibia miezi mitatu huku jumla ya wanafunzi milioni 15 kuanzia chekechea hadi vyuo vikuu wakiathirika.
Picha ya wanafunzi wakiwa darasani. Shughuli za masomo zilisitishwa kuzuia msambao wa COVID-19. Picha: UGC. Source: UGC
Kufikia sasa Uganda imesajili wagonjwa 705 wa COVID- 19, kulingana na ripoti ya wizara ya afya, huku 300 wakipata nafuu lakini bado hakuna kifo kilichoripotiwa kutokana na ugonjwa huo wa kupumua.
Humu nchini, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha alisema serikali inapanga kutoa maski kwa baadhi ya wanafunzi lakini watakaokosa watapata kutoka kwa wazazi wao.
“Kila mtoto shuleni lazima awe akivaa maski na serikali inafikiria kuhusu kuwapa maski lakini walio na uwezo wanafaa kuwanunulia wanao” alisema Magoha.
Magoha alisema serikali itajikakamua ili kuhakikisha wanafunzi shuleni wanapata maji, vyoo na hata vieuzi katika kukabiliana na covid-19.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.