Hatimaye Brian Kimani azikwa baada ya mwili wake kuzuiliwa hospitalini kwa miezi 4 Source: UGC
Hospitali hiyo iliamua kuachilia mwili wake juma lililopita na mwendazake amezikwa nyumbani kwao eneo la Ndenderu kaunti ya Kiambu.
Serikali iliipatia familia dakika 45 pekee kumzika mtoto huyo ikizingatiwa ni mojawapo ya masharti yaliowekwa na wizara ya afya ya kudhibiti kuenea kwa virusi vya ugonjwa wa corona.
“Serikali ilitupatia muda wa dakika 45 kumzika mtoto wetu, hii ni kwa ajili ya masharti yaliowekwa baada ya mlipuko wa virusi vya COVID-19, watu wachache waliruhusiwa kuhudhuria mazishi yake,” Alisema babake marehemu.