Jamaa mwenye umri wa miaka 32 ambaye alikuwa anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Mayanja, Bungoma kosa la ubakaji aliaga dunia Jumatatu, Juni 22 baada ya kushindwa kupumua.
Silvester Nyakundi, ambaye ni polisi katika kituo hicho pamoja na afisa mwenzake Jackline Muthoni walisema walisikia mlango wa seli hiyo ukibishwa saa kumi na moja asubuhi jinsi K24 iliripoti.
Picha ya mfungwa akiwa amezuiliwa ndani ya seli. Picha: The Standard. Source: UGC
“Walifungua seli na wakakuta wafungwa wengine wakijaribu kumsaidia mmoja wao, Jeremiah Namunyu, aliyekuwa amezirai baada ya kushindwa kupumua.
“OCS alifahamishwa na wakati alifika katika seli hiyo tayari mfungwa alikuwa ameaga dunia,” ilisema ripoti iliyoandikishwa katika kituo hicho chini ya OB 22/6/2020 ilisema.
Polisi walisema Namunyu alipaswa kuwasili mahakamani Jumatatu hiyo kujibu tuhuma za ubakaji dhidi yake.
Mwili wa mshukiwa ulipelekwa katika makafani ya hospiyali ya Rufaa ya Bungoma kufanyiwa upasuaji. Source: UGC
“Mtuhumiwa huyo alikuwa amepigwa na umati alipokamatwa, na alipokea matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Bungoma na kuruhusiwa kuondoka baada ya kupata nafuu,” ilisema ripoti hiyo iliongeza.
Mwili wa mshukiwa ulipelekwa katika makafani ya hospiyali ya Rufaa ya Bungoma kufanyiwa upasuaji.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.