– Video iliibuka mtandao ambapo wafanyikazi wawili wa hoteli wanashiriki usherati kazini bila haya
– Wanamtandao walidai kisa hicho kilikuwa kimefanyika katika mkahawa wa kifahari humu nchini
– Hata hivyo mkahawa wa Kempinski umekanusha madai hayo na kusema wawili hao ni si wafanyikazi wake
Mkahawa wa kifahari wa Villa Rosa Kempinski jijini Nairobi umetoa taarifa kuhusiana na video iliyodaiwa kuwa ya wafanyikazi wake.
Kempinski imekanusha madai kuwa video hiyo ambayo imesambaa mitandaoni ni ya wafanyikazi wake.

Mkahawa wa Villa Rosa Kempinski umekanusha madai kuwa video inayosambaa mntandaoni ya wafanyikazi wa hoteli wakishiriki penzi ilifanyika kwenye hoteli hiyo. Picha: Villa Rosa
Source: UGC
Kwenye taarifa Alhamisi, Juni 26, usimamizi wa mkahawa huo ulisema umepitia video hiyo na waliohusika si mojawapo wa wafanyikazi wake.
Uliwahakikishia wateja wake kuwa kitendo hicho pia hakikufanyika kwenye jengo lao kama ilivyokuwa ikidaiwa mtandaoni.
“Tungependa kufahamisha umma kuwa kuwa wawili hao si wafanyikazi wa Villa Rosa Kempinski, na tendo hilo pia halikufanyika katika mkahawa wetu,” taarifa ilisema.
Video hiyo ilionyesha wafanyikazi wawili wa hoteli wakiwa kazini kabla ya kushikwa na jazba na kuamua kula tunda kazini.
Wanapeana busu la mwaka kabla ya kuanza kushiriki penzi peupe katika kile kinaonekana kama eneo fiche la mkahawa.
Wawili hao wanafanya hivyo wakiwa wangali na mavazi yao ya kazini na hata nembo ya mkahawa wanaofanyia kazi inaonekana.

Mkahawa wa Kempinski umesema wawili hao wasihusishwe na hoteli hiyo.
Source: UGC
Tendo hilo lilinaswa na kamera za CCTV na wawili hao hawakujua kuwa siri ya usherati wao kazini itafichuka.
Upekuzi zaidi wa kanda hiyo umefichua kuwa huenda kisa hicho kilinakiliwa nchini Afrika Kusini.
Video hiyo ilifichuliwa kwanza na mwanamtandao anayejiita Waziri wa Mahaba.