– Waiguru alisema mumewe Kamotho Waiganjo ni ‘mume kutoka binguni’ kutokana na usaidizi anaompa
– Kamotho aliongoza kikosi cha mawakili wa Waiguru kwenye seneti kwenye kesi iliyoletwa na MCAs
– Kamati ya Seneti ilitupilia mashtaka yote dhidi ya gavana huyo na kusema mashtaka hayo hayakudhibitishwa
Gavana Ann Waiguru wa Kirinyaga amemtunuku mumewe sifa sifufu kwa kumtetea katika mashtaka yaliyokuwa yakimwandama katika Seneti.
Mumewe, Kamotho Waiganjo, aliongoza mawakili waliokuwa wakimtetea dhidi ya mashtaka yaliyoletwa na MCAs wa Kirinyaga.

Gavana Ann Waiguru alipokuwa Seneti wakati wa kuskizwa kwa kesi yake. Picha: Standard
Source: UGC
Gavana huyo alisema tofauti na akina mama wengine ambao wapenzi wao walikuja wakitembea, wake alitoka binguni.
“Natoa shukran za kipekee kwa mume wangu ambaye amekuwa akiniunga mkono kipindi hiki chote,” alisema gavana huyo.
“Rafiki yangu hivi karibuni aliniambia kuwa kuwa wapenzi kutoka binguni na wale ambao hujileta. Kwa kweli wewe ulitoka juu binguni,” aliongeza Waiguru

Wakili Kamotho Waiganjo. Waiganjo aliongoza kikosi cha mawakili wa Gavana Ann Waiguru. Picha: Nation
Source: Facebook
Katika Seneti, Waiganjo alijihami na kumtetea mpenziwe akipuuza ushahidi ulioleta na MCAs.
Alisema licha ya kuwa kulikuwa na madai kadhaa, hakuna hata moja ambalo lilikuwa limedhibitishwa kumhusisha Waiguru.
“Maseneta, angalau kunafaa kama kuna madai ya kupotea kwa pesa ionekana zilitolewa hapa na kuwekwa hapa na fulani ndiye alifaidika,” alisema Kamotho na kuitaka kamati ya seneti kutupilia mashtaka yote.

Wakili Kamotho Waiganjo. Waiganjo ni mumewe Gavana Ann Waiguru. Picha: Standard
Source: UGC
Waiganjo na Waiguru walioana mwezi Julai mwaka wa 2019 baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa muda.
Wawili hao walipeana talaka na wapenzi wao wa kwanza kabla ya kuingia kwenye uhusiano wao.