Makao makuu ya DCI katika barabara ya Kiambu. Picha: Daily Nation. Source: Twitter
Licha ya kwamba haijajulikana ni wapi kisa hicho kilirekodiwa, aliyesambaza video hiyo alisema kisa hicho kilitokea karibu na Ubalozi wa Thai, mtaani Kilimani.
Kwenye video hiyo, jamaa aliyekuwa amevalia shati jeupe, suti ya samawati na maski alionekana akiandamwa na jamaa wawili waliokuwa wamevalia jeketi za kofia.
Jamaa huyo alionekana kugutushwa baada ya mmoja wa watu hao kumtishia na bunduki kabla ya kuanza kumpekua mifukoni.
Mshukiwa wa pili naye anaonekana akimtishia jamaa huyo akiwa ameshikilia kisu huku akimuingia mifukoni na kumpokonya kilichokuwemo.