– Bob Orengo alihitimu na kujiunga na mawakili humu nchini baada ya kuapishwa Ijumaa, Julai 3
– ANajiunga na nyanja ambapo babake amekuwa na sifa sifufu kutokana na umahiri wake kwenye masuala ya kikatiba
– Bob amelelewa katika manthari ambapo baba na mama ni wanasheria sugu na hivyo atakuwa na kibarua kuafikia kiwango chao
Seneta wa Siaya James Orengo Ijumaa, Julai 3 alilala kwa furaha baada ya mwanawe kuhitimu na kujiunga na mawakili humu nchini.
Bob Orengo alikuwa miongoni mwa mawakili ambao waliapishwa na Jaji Mkuu David Maraga baada ya kuhitimu mitihani yao kwenye chuo cha mafunzo ya uanasheria.