Katika hali ya kuendelea kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corna, Rais Uhuru Kenyatta amesema kafyu ambayo imekuwapo itaendelea kawaida.
Akilihotubia taifa kuhusu mikakati iliyopo ya kukabiliana na maradhi ya Covid-19, rais alisema ni lazima kila mtu kuwa na tahadhari kubwa na kuzingatia maelekezi ya Wizara ya Afya kuhusu kuzuia kusambaa kwa virusi vya ugonjwa huo.
– Hakuna mikutano ya hadhara itakayoruhusiwa kwa siku 30 zijazo
– Maeneo ya kuabudia kufunguliwa kwa awamu na madrissa pamoja na shule za masomo ya dini kwa vijana makanisani kubakia ilivyokuwa awali
– Uchunguzi kuanzishwa kuhusiana na visa vingi vinavyoripotiwa vya dhulma za kijinsia, dhulma dhidi ya haki za watoto na visa vingi vya mimba za mapema miongoni mwa vijana ambao bado wanasoma katika shule za msingi na sekondari.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.