Waziri wa Uchukuzi James Macharia amesema kuwa abiria watakaotua nchini kutoka mataifa ya kigeni hawatalazimishwa kujiweka karantini
Hii ni iwapo hawataonyesha dalili zozote za ugonjwa hatari wa COVID-19 ambao umeangamiza mamilioni ya watu kote ulimwenguni.
” Abiria watakaowasili nchini watapimwa joto la mwili na iwapo kuna yeyote atapatikana akiwa na zaidi ya nyuzi joto 37.5, atatengwa mara hio hio,” Macharia aliasema.
Akizungumza na wanahabari akiwa katika jumba la Transcom jijini Nairobi, Macharia alisema hatua hiyo inanuia kuwavutia zaidi watalii ikizingatiwa wizara ya Utalii ameathirika sana kufuatia janga la ugonjwa wa Corona.
Aidha, Macharia aliongezea kuwa wahudumu wa ndege hawatalazimishwa kujiweka karantini endapo joto lao la mwili halitakuwa limezidi nyuzi joto 37.5. Source: Depositphotos