– Maabara ya Lancet imekuwa ikitoa matokeo tata ya maambukizi ya coronavirus
– Mutahi alisema hali hiyo inaendeleza dhana ya ripoti za serikali kushukiwa na Wakenya
– Hayo yametokana na ripoti kuwa wafanyakazi 18 wa shule moja Nakuru waliopimwa Lancet walipatikana na Covid-19 na kisha matokeo kubadilika
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe ameagiza uchunguzi kuanzishwa dhidi ya maabara ya Lancet Kenya kwa kutoa matokeo tatanishi ya Covid-19.
Kagwe alifichua hayo Alhamisi, Julai 17, wakati wa kikao na wanahabari kaunti ya Nakuru siku chache baada ya shule ya St Adrew’s Turi kuteta kuhusu matokeo ya wafanyakazi wake.
Waziri Mutahi Kagwe alisema maabara ya Lancet Kenya itachunguzwa. Picha: MoH Source: Facebook
Wafanyakazi 18 wa shule hiyo ya kifahari walipatikana na virusi vya Covid-19 baada ya kufanyiwa ukaguzi katika maabara ya Lancet.
Hata hivyo, hali ilibadilika baada ya ukaguzi mwingine kufanywa katika maabara ya KEMRI.
“Ni kweli kuna maabara moja ya Lancet ambayo matokeo yake yaligeuka. Na ni maabala hiyo pia ilikuwa na kisa kama hivho kwa watu fulani Nairobi,” alisema Kagwe.
Maabara ya Lancet jijini Nairobi. Maabala hiyo inadaiwa kutoa matokeo ya Covid-19 yanayokinzana na yale ya KEMRI. Picha: Standard Source: UGC
“Wizara itachukua hatua zake na pia tumeitaka bodi kuchukua hatua. Lakini pia nataka niwaombe msiende kwa maabala kama hiyo. Kwa nini uende maabara inayotoa matokeo tata? alisema Kagwe.
Kagwe alisema hawatakubali maabala kama hiyo kuendelea kuhudumu kwa sababu zinawafanya Wakenya kutilia shaka ripoti za ugonjwa wa coronavirus.
Shule ya St Andrew’s Turi ambapo wafanyakazi 18 walikuwa wamepatwa na coronavirus baada ya kukaguliwa katika maabala ya Lancet lakini mambo yakabadilika baada ya sampuli kupelekwa KEMRI. Source: UGC
Mbunge wa Molo alisema matokeo ya St Andrew’s yanaendelea kutilia shaka uhakika wa visa vinavyoripotiwa humu nchini.
“Ni afueni lakini pia inazua maswali mengi kuhusu matokeo yanayotolewa. Nitafuatilia hili kupitia wizara ya Afya,” aliongeza Kuria.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.