Connect with us

General News

Walevi wapumua – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na CHARLES WASONGA

ILIKUWA ni faraja kubwa kwa wahudumu wa mahoteli na vilabu vya burudani baada ya Rais Uhuru Kenyatta kutangaza Jumatano kuondolewa kwa amri ya kutotoka nje nyakati za usiku, almaarufu kafyu, ambayo ilitangazwa kuzuia kuenea kwa Covid-19.

Hii ina maana kuwa wafanyabiashara ambao huendesha shughuli zao nyakati za usiku sasa watakuwa huru kuendelea na kazi, wakiwemo wauza pombe na wateja wao.

“Kutokana na mamlaka niliyopewa kama Rais, naamuru kuondolewa kwa kafyu ambayo imedumu tangu Machi 27, 2020,” Rais Kenyatta akasema.

Alisema hayo alipoongoza sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Mashujaa katika uwanja Wang’uru, Kaunti ya Kirinyaga.

Kiongozi wa taifa alisema hatua hiyo inatokana na kupungua kwa idadi ya visa vya maambukizi yanayonakiliwa kila siku.

“Nilipohutubia taifa mnamo Juni 29, 2021 nilisema tunalenga kuhakikisha jumla ya Wakenya 10 milioni kufikia Desemba, 2021. Tumebaini kuwa kufikia sasa, jumla ya watu milioni 5 wamepewa chanjo. Hii ndio maana Baraza la Kitaifa la Kupambana na Covid-19 (NERC) na Baraza la Kitaifa la Usalama (NSC) wameamuru tutoe maagizo mapya kuhusu masharti ya corona,” akasema Rais.

Rais Kenyatta alionekana kuitikia presha kutoka kwa wanasiasa, wafanyabiashara na hata wataalamu wa afya waliomtaka afutilie mbali kafya hiyo kutokana na madhara yake kwa uchumi.

Miongoni mwa waliotoa shinikizo hizo ni kiongozi wa wa ODM Raila Odinga na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi.Rais Kenyatta pia alitangaza kuongezwa kwa idadi ya watu wanaoruhusiwa katika majumba ya ibada kutoka thuluthi moja hadi thuluthi mbili.

“Hii ni kutokana na kazi nzuri ambayo imefanywa na Baraza la Madhehebu Nchini. Pia nawapongeza Wakenya kwa kuendelea kuzingatia masharti ya kuzuia kuenea kwa corona na hivyo kuwa walinzi wa wenzao,” akasema.

Hata hivyo, alionya kuwa ugonjwa wa Covid-19 haujatokomezwa kabisa nchini na ipo haja ya Wakenya kuendelea kuzingatia masharti yaliyotolewa na Wizara ya Afya ya kuzuia maambukizi mapya.

Wakati huo huo, sekta za kilimo, elimu, afya na biashara ndizo zimepigwa jeki zaidi chini ya awamu ya tatu ya mpango uliotangazwa Rais Kenyatta jana kwa ajili ya kufufua uchumi kutokana na athari za janga la Covid-19.

Walevi wapumua – Taifa Leo
Rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margaret Kenyatta wakati wa Sherehe za Mashujaa Dei katika uwanja wa michezo wa Wang’uru, Kaunti ya Kirinyaga. Picha/ PSCU

Katika sekta ya kilimo, kiongozi wa taifa aliamuru Hazina ya Kitaifa kutoa mabilioni ya fedha kupiga jeki kilimo cha majani chai, kahawa, miwa na ufugaji ili kuwawezesha wakulima kupata faida.

Rais Kenyatta aliamuru Sh1 bilioni zitengewe sekta ndogo ya majani chai kununua mbolea kwa wakulima wadogo wa zao hili.

“Hii itawapunguzia wakulima gharama ya uzalishaji na hivyo kuwawezesha kupata faida,” akasema alipoongoza taifa katika sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Mashujaa katika uwanja wa michezo wa Wang’uru, Kaunti ya Kirinyaga.

Rais Kenyatta pia aliamuru kutengwa kwa Sh1.5 bilioni za kulipa wakulima wa miwa ambazo wanadai kampuni za kutengeneza sukari zinazomilikiwa na serikali.

“Fedha hizi pia zitatumika kugharamia ukarabati wa mitambo katika kampuni za miwa ambazo ziko chini ya usimamazi wa serikali,” akasema kwenye sherehe hiyo iliyohudhuriwa Rais wa Malawi Dkt Lazarus Chakwera, Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ODM Raila Odinga na viongozi mbalimbali.

Rais Kenyatta vile vile alitangaza kuwa Sh1.5 bilioni kwa sekta ya ufugaji kufadhili mpango wa ununuzi wa mifugo ambao wameathirika na janga la ukame haswa katika maeneo kame nchini.

Katika sekta ya elimu, kiongozi wa taifa ameamuru Hazina ya Kitaifa itoe Sh8 bilioni madarasa 10,000 zaidi kote nchini ili kukidhi mahitaji ya wanafunzi ambao watajiunga na Gredi 6.

“Madarasa haya yatajengwa na wanandarasi wa humu nchini ili kuinua chumi za maeneo ya mashinani,” Rais Kenyatta akaeleza.

Vile vile, kiongozi wa taifa alitangaza kuwa serikali itajenga hospitali 50 za hadhi ya Level 3 katika maeneo mbalimbali nchini kama sehemu ya kufanikisha maono yake ya Afya kwa Wote (UHC) ambayo ni mojawapo ya Ajenda Nne za Maendeleo.

“Hospitali hizi zitajengwa kwa gharama ya Sh3.5 bilioni na wakandarasi wa humu nchini,” Rais Kenyatta akafafanua.

Wakati huo huo, Rais alitangaza kuwa gharama ya umeme itapunguzwa kwa asilimia 30 kufikia Desemba 24, mwaka huu.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending