Connect with us

General News

Maroon young stars miaka sita ijayo inalenga kutinga ligi kuu nchini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Na JOHN KIMWERE 

MAROON Youngstars itakuwa kati ya vikosi vitakavyokuwa vikishiriki kwa mara ya pili mechi kuwania taji la Nairobi West Regional League (NWRL) muhula ujao.

Maroon Youngstars ya kocha, Mohamed Amin ilikuwa kati ya timu 14 zilizokuwa zimepangwa Kundi A kwenye mechi za ngarambe hiyo msimu uliyopita.

”Ingawa ni miaka michache tangia uunde timu hii ambapo wachezaji wetu bado wanajikuza katika mchezo wa kandanda tunaamini tumekaa vizuri kufanya kweli kwenye kampeni za kipute cha msimu ujao,” kocha huyo alisema na kuongeza kuwa wanafahamu bayana hakuna mteremko kwenye kinyang’anyiro hicho.

Kocha huyo anashikilia kwenye mechi za msimu ujao hawatakuwa na la ziada bali watakuwa tayari kupambana mwanzo mwisho ili kutimiza amza yao kubeba taji hilo na kupandishwa ngazi kushiriki Ligi ya Taifa Daraja la Pili.

Maroon chini ya nahodha, Abdi Ibrahim iliteleza na kumaliza ya saba kwenye jedwali kwa kusajili alama 32, sawa na Silver Bullets. Nayo Uthiru Vision ilifunga tisa bora ikiwa ya mwisho kati ya vikosi vilivyojikatia tiketi ya kusalia kushiriki ngarambe hiyo msimu ujao.

Maroon young stars miaka sita ijayo inalenga kutinga ligi kuu nchini – Taifa Leo
RE UNI: Baadhi ya wachezaji wa Re Union FC ambayo hushiriki kipute cha NWRL…Picha/JOHN KIMWERE

 

MAKARIOS 111 FC 

Anasema kuwa kwenye kampeni za muhula ujao wanatarajia ushindani mkali kutoka kwa washiriki wengine kama Makarios 111 (Riruta United), Melta Kabiria  na Escalators FC kati ya zingine.

Kama ilivyo kawaida kwa timu nyingi, Maroon Young Stars inajipatia miaka sita kuhakikisha imetwaa tiketi ya kufuzu kushiriki ngarambe ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF-PL).

Pia viongozi hao wanashikilia kuwa wanatamani kuibuka mabingwa wa kipute hicho na kujikatia tiketi ya kuwakilisha taifa hilo kwenye mechi za Shirikisho la Afrika (CAF).

”Hata hivyo tunalenga kutimiza hayo hatua kwa hatua hatuna maana timu za soka zinazidi kuimarika katika soka kila kuchao,” naibu wa kocha wa kwanza, Abdul Abdi alisema.

Naye naibu wa kocha wa pili, Ali Sifuma anasema timu hiyo ina wachezaji kadhaa ambao tayari wameonyesha dalili za kufuzu kushiriki soka la kimataifa miaka ijayo.

”Sina shaka kutaja kuwa tuna chipukizi kadhaa ambao tayari wameonyesha wazi kuwa miaka michache ijayo watafuzu kuchezea timu ya taifa ya Harambee Stars,” akasema.

Kati ya wachezaji hao ni Lawrence Ijaka, Simon Bryan, Imram Granton na Omar Mandi kati ya wengine. Inajivunia kunoa makucha ya wachezaji wawili wanaochezea klabu za kipute cha FKF-PL.

Wachana nyavu hao ni RichDonald Bolo (Western Stima) na Teddy Pkiach (Gor Mahia FC).

 

LANG’ATA BARRACKS

Maroon Youngstars yenye makazi yake kwenye kambi ya Lang’ata Barracks iliasisiwa mwaka 2018 na wachezaji kadhaa baada ya kumaliza elimu ya sekondari. Inajumuisha wachezaji 18 ambao ni wanao maofisa wa jeshi la Kenya ambao huishi katika kambi hiyo.

Pia inasaini chipukizi 12 kutoka mitaa jirani ya Camp David Estate, Karen na Rongai .Kwenye jitihada za kunoa vipaji vya wachezaji wake timu hii inajivunia kushiriki na kufanya vizuri kwenye mashindano mbali mbali tangia ibuniwe.

Imeshinda mataji kama Inter Army Garrisson 2018, Rorie Tournament 2019 na Ajab Unga Tournament 2021. Pia kwenye mechi za Two Rivers Tournament na Ole Kasasi Cup ilimaliza nafasi ya tatu na pili mtawalia.

REFA;Baadhi ya waamuzi ambao huchezesha mechi za NWRL…Picha/JOHN KIMWERE

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending