[ad_1]
TAHARIRI: Pamoja na ole
MANCHESTER, Uingereza
Gunge Cristiano Ronaldo anaunga mkono Ole Gunnar Solskjaer kuendelea kuwa kocha mkuu wa Manchester United, tetesi zinadai.
Nambari saba United itakabiliana na Tottenham Hotspur inayoshikilia nafasi ya sita hapo kesho.Ingawa mshambuliaji huyo anadhaniwa kuwa tatizo kambini Old Trafford na hapendezwi na baadhi ya mbinu za Solskjaer na anavyochagua kikosi cha siku ya mechi, supastaa huyo amesihi wachezaji wenzake waendelee kumpa kocha huyo usaidizi anaohitaji kwa kuonyesha viwango vya juu vya uchezaji.
Solskjaer anakabiliwa na presha kutokana na msururu wa matokeo duni.Shinikizo liliongezeka dhidi ya kocha huyo kutoka Norway baada ya ‘mashetani wekundu’ wa United kukosa pa kujificha walipomiminiwa mabao 5-0 na maadui wakuu Liverpool mnamo Oktoba 24.
Solskjaer anaaminika kupewa mechi tatu tu (dhidi ya Tottenham na Manchester City ligini na Atalanta kwenye Klabu Bingwa Ulaya) kujiokoa ugani Old Trafford.Kwenye kipute cha Carabao ni kuwa mabingwa Manchester City walibanduliwa na West Ham kwa njia ya penalti 5-3 baada ya muda wa kawaida kumalizika 0-0 jijini London.
City walikuwa wameshinda Carabao miaka minne mfululizo.Leicester ililemea Brighton 4-2 kwa njia ya penalti ugani King Power baada ya dakika 90 kukatika 2-2, Brentford ilibandua wenyeji Stoke 2-1, nao Divock Origi na Takumi Minamino wakafungia wageni Liverpool katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Preston.
Wageni Tottenham walinyoa Burnley bila maji 1-0. Mechi hizo zilikuwa za kuingia robo-fainali ambayo droo yake itafanywa Oktoba 30. Aidha, Oktoba 27 ilikuwa siku mbaya kwa miamba Bayern Munich, Juventus na Barcelona.
Bayern aliaibishwa 5-0 na Borussia Monchengladbach kwenye raundi ya tatu ya kipute cha DfB Pokal, Barcelona wakang’atwa na Rayo Vallecano kwenye La Liga nao Juventus wakazimwa 2-1 na Sassuolo kwenye Serie A
[ad_2]
Source link