Connect with us

General News

Walioteketeza shule watozwa Sh50,000 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Walioteketeza shule watozwa Sh50,000 – Taifa Leo

Walioteketeza shule watozwa Sh50,000

GEORGE MUNENE Na ALEX NJERU

WANAFUNZI sita walioshutumiwa dhidi ya kuteketeza bweni nne na kuharibu mali yenye thamani ya Sh11.1milioni walishtakiwa jana kwa kosa la kuteketeza mali kimaksudi katika mahakama ya Baricho, Kaunti ya Kirinyaga.

Walishutumiwa kwamba mnamo Oktoba 24, 2021 katika Shule ya Sekondari ya Kibirigwi Girls, eneo la Ndia, waliteketeza majengo na kusababisha taasisi hiyo ya elimu kufungwa.Walikanusha mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkuu C. Korir na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh50,000 kila mmoja hadi Novemba 8, wakati kesi hiyo itakapotajwa.

Korti ilielezwa kuwa siku ya tukio hilo, mwendo was aa tatu usiku, bweni hizo zilizokuwa makao kwa wasichana 213, ziligeuzwa majivu.=

Mali iliyojumuisha magodoro, vitabu, blanketi, mifuko na sare za wasichana hao pia iliteketezwa.Katika Kaunti ya Tharaka Nithi, polisi wanachunguza shule mbili za wavulana zinazokaribiana zilizoteketezwa wakati sawa Jumapili iliyopita.

Naibu Kamishna wa Maara Philip Sigei alieleza vyombo vya habari kuwa sadfa hiyo ni suala tata katika uchunguzi unaoendelea kuhusu kuteketezwa kwa bweni hizo mbili katika Shule ya Upili ya Kiriani Boys na katika Shule ya Upili ya Muthambi Boys.

Polisi wanashuku huenda kulikuwa na mawasiliano kati ya wahusika wa visa hivyo viwili.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending