Connect with us

General News

Hisia mseto Mbagathi Road ikiitwa Raila Odinga Way – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Hisia mseto Mbagathi Road ikiitwa Raila Odinga Way – Taifa Leo

Hisia mseto Mbagathi Road ikiitwa Raila Odinga Way

Na MARY WANGARI

BARABARA ya Mbagathi katika Kaunti ya Nairobi hatimaye imebadilishwa jina na kuitwa Raila Odinga Way kwa heshima ya kiongozi wa ODM.

Hata hivyo, hatua hiyo imeibua hisia mseto miongoni mwa Wakenya.

Mkurugenzi wa Mawasiliano katika Kaunti ya Nairobi, Jacob Elkana, alithibitisha hatua hiyo ya Alhamisi, akisema aliyekuwa waziri mkuu anastahili kutuzwa kwa sababu amekuwa akiwapigania Wakenya kwa muda mrefu.

Baadhi ya Wakenya waliipongeza, na wengine kuikosoa.

Waliounga mkono walisema hatua hiyo imejiri wakati mwafaka na ni heshima kuu kwa kiongozi wa ODM wakihoji kuwa anastahili tuzo kuu hata zaidi kwa mchango wake katika kutetea haki za kidemokrasia nchini.

Waliopinga hatua hiyo walisema Bw Odinga pamoja na wanasiasa wengine hawastahili kuenziwa kwa sababu wamekuwa wakijinufaisha kwa jasho la Wakenya raia wakiumia.

“Mbona tunaheshimu wezi katika enzi na kizazi hiki,” alishangaa Nahashon Kimemia.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending