Connect with us

General News

Real Madrid yakung’uta Rayo Vallecano na kutua kileleni mwa jedwali la La Liga – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Real Madrid yakung’uta Rayo Vallecano na kutua kileleni mwa jedwali la La Liga – Taifa Leo

Real Madrid yakung’uta Rayo Vallecano na kutua kileleni mwa jedwali la La Liga

Na MASHIRIKA

REAL Madrid walirejea kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) baada ya kusajili ushindi wa 2-1 dhidi ya Rayo Vallecano uwanjani Santiago Bernabeu.

Toni Kroos aliwaweka wenyeji Real kifua mbele kunako dakika ya 14 baada ya kukamilisha krosi ya Vinicius Junior.

Karim Benzema alifanya mambo kuwa 2-0 kabla ya kipindi cha kwanza kutamatika. Goli hilo la Benzema lilikuwa lake la 10 hadi kufikia sasa ligini na lilitokana na krosi safi ya beki David Alaba.

Radamel Falcao alitokea benchi katika kipindi cha pili na kufungia Vallecano bao la kufutia machozi katika dakika ya 77.

Ushindi wa Real uliwapaisha hadi kileleni mwa jedwali la La Liga kwa alama 27, mbili zaidi kuliko nambari mbili Real Sociedad. Vallecano kwa sasa wanakamata nafasi ya sita kwa pointi 20.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending