Connect with us

General News

Nebulas wafinya Little Prince vikapu vya Ligi ya Kitaifa daraja la pili wanaume – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Nebulas wafinya Little Prince vikapu vya Ligi ya Kitaifa daraja la pili wanaume – Taifa Leo

Nebulas wafinya Little Prince vikapu vya Ligi ya Kitaifa daraja la pili wanaume

Na TITUS MAERO

Wanavikapu Nebulas walisajili ushindi wa 68-61 dhidi ya Little Prince ya Nairobi kwenye mechi ya Ligi ya Kitaifa Daraja ya Pili mpira wa vikapu kwa Wanaume.

Mchuano huo wa Shirikisho la Vikapu Nchini (KBF) ulisakatwa mjini Kakamega mnamo Jumamosi.Nebulas ya mkufunzi Joseph Koech ilijitahidi na kushinda robo ya kwanza 11-10, ikalemewa ya pili 17-12, ikatoka sare 18-18 robo ya tatu kabla kuchomoka na ya nne 27-16.

Little Prince chini ya kocha Oliver Onyango ilikuchota robo ya pili 17-12 katika mchuano huo.Madume wa Little Prince waliongoza 27-23 kufikia muda wa mapumziko wa pambano hilo la kusisimua.Nahodha wa Little Prince Henry Opondo aliongoza kikosi chake kulazimishia wenyeji sare ya 18-18 kwenye robo ya tatu.

Aidha, bidii ya mchwa ya Nebulas wakiongozwa na Nahodha wao Stephen Omondi, iliwawezesha kuchomoka na robo ya nne 27-16.Na Titus Maero

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending