Connect with us

General News

Naibu Rais Dkt Ruto kuzuru ngome ya Raila ya Luo Nyanza – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Naibu Rais Dkt Ruto kuzuru ngome ya Raila ya Luo Nyanza – Taifa Leo

Naibu Rais Dkt Ruto kuzuru ngome ya Raila ya Luo Nyanza

Na CHARLES WASONGA

NAIBU Rais William Ruto atafanya ziara ya siku tatu katika ngome ya kiongozi wa ODM William Ruto katika kaunti ya Kisumu.

Kulingana na ratiba iliyotolewa na mshirikishi wa chama cha United Democratic Alliance (UDA) Eliud Owalo, ziara ya Dkt Ruto itaanza katika eneo la Kondele. Atatoa zawadi ya basi kwa kundi la Vijana wa Kondole kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika soko la Kondole.

Baadaye Dkt Ruto atafulululiza hadi eneo la Nyahera katika eneo bunge la Kisumu Magharibi ambapo atatoa michango ya fedha kuyasaidia makundi na akina mama na wahudumu wa boda boda. Atakamilisha siku yake ya kwanza kwa kutembelea Shule ya Msingi ya Nyalunya ambako anatarajiwa kutoa zawadi ya basi.

Mnamo Jumatano, Dkt Ruto atazuru kaunti ya Migori ambapo atapokelewa na Gavana wa kaunti hiyo Okoth Obado. Baadaye atakamilisha ziara yake katika Luo Nyanza kwa kutembelea kaunti ya Homa Bay mnamo Alhamisi.

Bw Owalo alisema kuwa Naibu Rais atapanga ziara yake katika kaunti ya Siaya “hivi karibuni ili mahasla wa sehemu hiyo wasiachwe nyumba katika mpango huu wa kuboresha uchumi kutoka mashinani.” Ziara ya Dkt Ruto katika kaunti za Luo Nyanza inajiri siku chache baada yake kufanya ziara ya siku mbili katika kaunti jirani za Kisii na Nyamira kusaka uungwaji mkono.