[ad_1]
Shirika la ndege kutumbuiza wateja wake wakiwa safarini
Na BENSON MATHEKA
KAMPUNI YA safari za ndege ya Jambojet, imetangaza kuwa imeanzisha huduma za kuburudisha wateja wake wakiwa safarini (IFE).
Kupitia huduma hiyo itakayotekelezwa kwa ushrikiano na Global Onboard Partners, wateja wataweza kupata video na muziki kutoka kwa kijisanduku cha IFE kupitia simu za mkono na vifaa vingine vya elektroniki kama vile laptopu wakiwa ndani ya ndege.
“Wateja hutumia saa moja katika safari. Mfumo wa kuwaburudisha wakiwa ndani ya ndege utahusu video, michezo na vifaa vya kusoma wakiwa safarini,” alisema Bw Karanja Ndegwa, Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mkuu Mtendaji wa Jambojet.
“Huduma hiyo pia inatoa nafasi kwa mashirika ya kibishara na kampuni zinazotaka kuweka matangazo kuvumisha bidhaa na huduma zao kupitia mfumo huo kwa kutumia video au picha,” alisema.Afisa Mkuu Mtendaji wa Global Onboard Partners Kirk Adams, alisema wanafurahi kushirikiana na Jambojet.
“Jukwaa letu la ubunifu limeundwa kutoa ushindi kwa kila mtu kupitia burudani kwa wateja hadi wanakoenda na kupitia njia mpya za mapato kwa kampuni za ndege.”Kwa wakati huu Jambojet inasafiri hadi Mombasa, Eldoret, Kisumu, Malindi, Lamu na Ukunda (Diani) kutoka Nairobi.
Kampuni hiyo pia ina safari za ndege hadi mji wa Goma, Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.Kampuni hiyo imekuwa ikikua kwa kipindi cha miaka saba ambayo imekuwa ikiendesha huduma zake nchini Kenya ikitoza ada afueni kwa wateja wake.
Next article
Miradi ya kisasa yatia uchungu ‘Lamu tamu’
[ad_2]
Source link