Huenda ahadi za wanasiasa ni maneno matamu tu
Na KIPKOECH CHEPKWONY
WANASIASA watakaoshiriki kwenye kinyag’anyiro cha Urais 2022 sasa wameanza kuuza sera zao kila upande nchini huku wakiahidi wanainchi namna wataleta nafuu serikalini iwapo watapigiwa kura kwenye uchaguzi ijayo.
Baadhi ya viongozi hao tayari washaanza msururu wao wa kutembelea wanainchi kwa maeneo mbalimbali wakiuza sera zao. Hotuba zao mara nyingi huwa na hoja kadhaa hoja hizi ni muhtasari wa mawazo makuu ya kampeni na hurudiwa mara kwa mara ili kujenga hisia tu ya kudumu kwa wapiga kura.
Ahadi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga ya Sh 6,000 kila mwezi kwa kwa famila ya Wakenya walio katika hali hatarini iwapo atachaguliwa kuwa rais katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao Ina jumla ya bajeti takriaban billion 144 kila mwaka. Wengi wametibua mashimo katika ahadi hiyo, akiwemo kiongozi wa chama cha Amani National Congress (ANC) Musalia Mudavadi ambaye anasema haitakuwa jambo la busara, ikizingatiwa idadi ya vijana wasio na kazi na rekodi za mauzo duni za Kenya kwa njia ya ushuru.
“Tunapokaribia Uchaguzi Mkuu ujao, lazima tuipe nchi hii yaliyo mema, tusishawishike kwa takrima, hongo au maneno matamu kutoka kwa wanasiasa wanaokuahidi mambo ambayo kiuhalisia hayawezekani,” alisema Mudavadi. Raila, ambaye amekuwa akitangaza pesa hizo kwa muda wa miezi kadhaa iliyopita, alibainisha kuwa zaidi ya milioni 8 watafaidika na mpango huo.
“Wengine wanauliza hizo 6,000 za familia maskini zitatoka wapi. Nataka kuwaambia nimekuwa waziri mkuu wa nchi hii, najua pesa hizo ziko wapi,” Raila alisema katika ziara yake Lamu Jumapili. Naibu Rais William Ruto naye ameahidi kujumuisha Ajenda Nne Kuu za Rais Uhuru Kenyatta kupitia muundo wake wa kiuchumi wa chini kwenda juu Bottom up Economy ili kuhakikisha maendeleo kote nchini.
Hii ni pamoja na kuinua hali ya maisha kwa wakenya ambao wana biashara ndongo kama vile wamama mboga, wanabodaboda na vijana kupata ajira nchini. “ukosefu wa ajira ndio changamoto kuu inayokabili nchi ambayo lazima ikabiliwe kimkakati,” Dkt Ruto alisema.
Ruto alitaja kuwa serikali ya Hustler Nation itawekeza katika miradi na mipango ambayo itaunda nafasi za kazi na kupunguza ukosefu wa ajira. “Programu ya ujenzi wa nyumba, ambayo ilikuwa sehemu ya ajenda Nne Kuu ambayo tangu wakati huo imevurugwa na Upinzani, ingetengeneza nafasi za kazi milioni 2 kufikia sasa,”Naibu Rais William Ruto alikariri akiwa kwenye mkutano eneo la Nyanza.