Connect with us

General News

‘Siku ya Wajinga’ inavyoakisi taswira za uana katika jamii – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

‘Siku ya Wajinga’ inavyoakisi taswira za uana katika jamii – Taifa Leo

JUNGU KUU: ‘Siku ya Wajinga’ inavyoakisi taswira za uana katika jamii

Na BITUGI MATUNDURA

MAJUMA mawili yaliyopita, niliangazia jinsi taswira dumifu za uana zinavyobainika katika kazi ya Razwana Kimutai – Ndoto ya Riziki (Oxford University Press).

Katika makala ya leo, ninahakiki kazi ya Siku ya Wajinga (Phoenix). Hii ni mojawapo ya kazi za kisanaa za Clara Momanyi.

Prof Momanyi ni mtunzi wa hadithi fupi na riwaya za vijana.

Baadhi ya tungo zake ni pamoja na Tumaini (2006), Nguu za Jadi (Queenex) na Nakuruto (Longhorn).

Jagina katika Siku ya Wajinga ni Zito ambaye ni mwanafunzi katika shule ya Msingi ya Kambini.

Zito ni mtundu na mwenye mizaha mingi darasani.

Tofauti na rafikize, Sadiki na dada yake Zena ambao ni wenye bidii za mchwa masomoni, Zito ni mvivu.

Mienendo hii yake inamtia matatani kila mara na kusababisha aadhibiwe na wazazi wake na walimu mara kwa mara.

Zito ana falsafa kwamba ‘werevu ukikushinda jaribu ujinga’.

Katika kuitetea falsafa yake hii, Zito anafanya juhudi kuwashawishi wanafunzi wenzake kuamini kwamba mtu mwerevu daima humtumikia mtu mjinga.

Zito ameukumbatia ujinga kwelikweli.

Kutokana na uzembe wake, Zito hang’amui somo la Hisabati wala hataki kusaidiwa na wanafunzi wenzake wanaojitolea kumsaidia katika somo hilo hasa wasichana.

Licha ya kutopenda somo hilo, Zito pia hampendi mwalimu Petro ambaye analifunza somo lenyewe.

Mwalimu Petro anamwadhibu Zito mara kwa mara kwa sababu ya kufeli somo hilo.