Connect with us

General News

3 walazwa hospitalini Marsabit baada ya kushambuliwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

3 walazwa hospitalini Marsabit baada ya kushambuliwa

3 walazwa hospitalini Marsabit baada ya kushambuliwa

Na JACOB WALTER

WATU watatu wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Marsabit wakiwa na majeraha ya risasi baada ya kushambuliwa nyumbani kwao eneo la Kiwanja Ndege, Ijumaa.

Watatu hao, mwanamume, mwanamke na mtoto, walishambuliwa mwendo wa saa kumi alifajiri na watu wasiojulikana waliotoroka kwa pikipiki.

Naibu Kamishna wa Kaunti ya Marsabit David Saruni alisema maafisa wa usalama wangali wanawafuata washambuliaji hawa wawili ambao inaaminika walitorokea upande wa eneo la Dakabaricha.

“Tunafanya kila tuwezalo kuwakamata wahalifu hao ili wafunguliwe mashtaka. Naomba wanajamii kutofanya mashambulio ya kilipiza kisasi ambayo yanaweza kugeuza hali kuwa mbaya zaidi. Wakazi sharti waelewe kwamba pikipiki za uchukuzi wa abiria zimepigwa marufuku kuhudumu katikati mwa mji wa Marsabit. Marufuku hiyo iliwekwa mnamo Novemba 6 na Makati ya usalama katika kaunti,” akasema Bw Saruni.

Marufuku hiyo iliwekwa baada ya uchunguzi kubaini kuwa visa vingine vya watu kuawa mjini Marsabiti vilitekelezwa na watu waliokuwa wakisafiri kwa pikipiki.

Kisa cha hivi punde kilifanyika Jumatano ambapo mtu moja aliuawa na mwingine akajeruhiwa kwa kushambuliwa na watu wasiojulikana na waliokuwa wakisafiri kwa pikipiki.

Tafsiri: CHARLES WASONGA

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending