Connect with us

General News

Mganda avunja rekodi ya dunia mbio za kilomita 21 iliyoshikiliwa na Mkenya Kandie – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Mganda avunja rekodi ya dunia mbio za kilomita 21 iliyoshikiliwa na Mkenya Kandie – Taifa Leo

Mganda avunja rekodi ya dunia mbio za kilomita 21 iliyoshikiliwa na Mkenya Kandie

Na GEOFFREY ANENE

MTIMKAJI Jacob Kiplimo amevunja rekodi ya dunia ya mbio za kilomita 21 ya Mkenya Kibiwott Kandie kwenye mbio za EDP Lisbon Half Marathon nchini Ureno mnamo Jumapili.

Mganda huyo mwenye umri wa miaka 20 amekamilisha umbali huo kwa dakika 57:31 akifuta rekodi ya Dunia, Afrika na Kenya ya 57:32 iliyoshikiliwa na Kandie tangu Desemba 6, 2020 aliposhinda taji la Valencia Half Marathon nchini Uhispania.

Kiplimo, ambaye ni Mganda wa kwanza katika historia ya Half Marathon kumiliki rekodi ya dunia ya kilomita 21, alikimalisha dakika mbili mbele ya wapinzani wake wa karibu Huseydin Mohamed Esa (Ethiopia) 59:39, Gerba Beyata Dibaba (Ethiopia) 59:39, Hillary Kipkoech (Kenya) 59:41, Ibrahim Hassan Bouh (Djibouti) 59:41 na Milkesa Menhgesa Tolosa (Ethiopia) 59:48.

Taji lake kinadada, ambalo Mkenya Vivian Cheruiyot alishinda mwaka 2019 wakati mbio hizi zilifanyika mara ya mwisho, limenyakuliwa na Muethiopia Tsehay Gemechu Beyan (saa 1:06:06).

Wakenya Daisy Cherotich (1:06:15) na Joyce Chepkemoi Tele (1:06:19) waliridhika na nafasi ya pili na tatu mtawalia. Hiwot Bebrekidan Bebremaryam (Ethiopia) 1:08:00, Vibian Chepkirui (Kenya) 1:08:02 na Ethlemahu Sintayehu Dessi (Ethiopia) 1:08:16 wametamatisha mduara wa sita-bora.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending