Connect with us

General News

Wadhifa wa Mwakilishi wa Kike Kaunti wakosa kuvutia wawaniaji – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wadhifa wa Mwakilishi wa Kike Kaunti wakosa kuvutia wawaniaji – Taifa Leo

Wadhifa wa Mwakilishi wa Kike Kaunti wakosa kuvutia wawaniaji

Na LUCY MKANYIKA

IDADI ya wanawake wanaotaka kuwania nafasi ya Mbunge Mwakilishi wa Kike Kaunti ya Taita Taveta, imeendelea kuwa ya chini mno huku siasa za 2022 zikizidi kushika kasi.

Kufikia sasa, mwanamke mmoja pekee ndiye ametangaza nia ya kumbandua Bi Lydia Haika katika nafasi hiyo.

Bi Esther Mwanyumba ambaye ni Waziri wa Maji katika Kaunti, amekuwa akipigiwa upato na Gavana Granton Samboja.’Kwa sasa ninashikilia afisi ya serikali kwa hivyo sitaki kuchanganya na siasa.

Nitapiga siasa kampeni zitakapotangazwa mwaka ujao,’ Bi Mwanyumba aliambia Taifa Leo.Hata hivyo, kiti cha ugavana kimevutia wanawake kadhaa akiwemo Bi Patience Nyange na Bi Rachel Mwakazi Skjaerpe.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending