Connect with us

General News

Utakosa huduma za serikali na mikahawani ikiwa haujapata chanjo ya corona, Kagwe aonya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Utakosa huduma za serikali na mikahawani ikiwa haujapata chanjo ya corona, Kagwe aonya – Taifa Leo

Utakosa huduma za serikali na mikahawani ikiwa haujapata chanjo ya corona, Kagwe aonya

Na CHARLES WASONGA

WIZARA ya Afya imetangaza kuwa watu ambao hawajapokea chanjo ya kuzuia maambukizi ya Covid-19 huenda wakanyimwa huduma katika asasi za serikali.

Akiongea na wahabari Jumapili katika makao makuu ya wizara yake, Nairobi, Waziri Mutahi Kagwe aliongeza kuwa wateja wa mikahawa, mabaa na magari ya uchukuzi wa umma pia watahitaji kuwa na cheti cha kuonyesha kuwa wamepokea chanjo ya corona kabla ya kupewa huduma.

“Hii ndio njia itakayohakikisha kuwa serikali haifungi nchi tena baada ya idadi ya maambukizi ya corona kupanda. Kufikia Desemba ni watu waliopata dozi mbili za chanjo ya AstraZeneca, Pfizer au Moderna na dozi moja ya chanjo aina ya Johnson and Johnson ndio watapata huduma katika afisi za serikali,” Bw Kagwe akasema alipotoa taarifa kuhusu hali ya maambukizi ya Covid-19 nchini.

Waziri Kagwe ambaye alikuwa ameandamana na mwenzake wa Utalii Najib Balala alitisha kuwa wamiliki wa mikahawa, mabaa na baa ambao watahudumia wateja wasio na ithibati kuwa wamepata chanjo watapokonywa leseni ya kuhudumu.

“Aidha, ningependa kuwatangazia Wakenya kuwa madereva wa magari ya uchukuzi na wahudumu wa boda boda watahitajika uonyeshe ithibati kuwa umepata chanjo kabla ya wao kukusafirisha.” akasema.

Bw Kagwe alisema maafisa wa Wizara ya Uchukuzi na wadau wengine katika sekta hiyo watahakikisha kuwa agizo hilo limetekelezwa haswa katika msimu wa sherehe za Krismasi na Mwaka Mpya.

Alisema wahudumu wote katika sekta ya uchukuzi sharti wahakikishe wamepata chanjo ya kuzuia kusambaa kwa Covid-19.

“Vile vile, wageni kutoka mataifa ya ng’ambo wanaokuja Kenya watahitaji kuonyesha cheti cha kuonyesha wamepata chanjo hii ndiposa wapate idhini ya kuingia nchini.” Bw Kagwe akaeleza.

Mataifa ya Uhispania, Ujerumani, Denmark na Israeli ni miongoni mwa yale ambayo yanatekeleza sharti hili.