[ad_1]
Polisi wakosa kunasa wezi wa benki Kisumu
ELIZABETH OJINA na VICTOR RABALLA
JUHUDI za maafisa wa polisi kuwanasa majambazi walioteka tawi moja la Benki ya Equity mjini Kisumu ziliambulia patupu baada ya operesheni ya saa tatu.
Duru za polisi zilisema wezi hao waliingia katika jengo la benki hiyo katika barabara ya Ang’awa saa tano unusu za asubuhi.Kamanda wa polisi eneo la Nyanza, Magu Mutindika alisema mmoja wa washukiwa alifika kwa kashia akidai Sh100,000, la sivyo amuue.
“Kashia alishtuka na kuchangia washukiwa wenzake kutoroka huku wateja wakikimbilia usalama,” akawaambia wanahabari.Maafisa wa polisi wanaotoa ulinzi katika jengo hilo walifunga lango kuu kwa haraka, hatua iliyopelekea mshukiwa huyo kurusha mkebe wa gesi ya kutoa machozi.
Alielekea sehemu ya juu ya jengo hilo.Picha za kamera za usalama, CCTV, zilimwonyesha mwanamume huyo akibadilisha shati kabla ya kuteremka chini na kutoroka pamoja na wateja wengine katika sokomoko hizo.
“Tumehifadhi shati hilo. Vile vile, tutafanya uchunguzi zaidi kwa kuwahoji baadhi ya watu ambao tumewakamata walipokuwa wakitoroka kutoka eneo la tukio,” Bw Mutundika akasema muda mfupi baada ya kusitisha msako saa nane na dakika 38 mchana.
Mkuu huyo wa polisi alifichua kwamba, baadhi ya watu wanaozuiliwa kuhusiana na kisa hicho ni wafanyakazi wa benki hiyo na wateja waliokuwa kuwepo wakati wa jaribio hilo la wizi.“Tunataka kufanya uchunguzi mkali na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu yeyote ambaye atapatikana kuhusika katika uhalifu huo,” Bw Mutundika akasema.
Next article
Wageni wakoroga starehe za vigogo wa zamani ODM
[ad_2]
Source link