Hesabu ngumu za Man-U kumleta Poch’ Old Trafford
MANCHESTER, UINGEREZA
Na MASHIRIKA
KLABU ya Manchester United inasaka mkufunzi wa muda atakayesimamia timu hadi msimu wa sasa umalizike, huku wakiendelea kuwinda kocha wa kudumu.
Kocha Mauricio Pochettino amesema yuko tayari kuajiriwa na mibabe hao wa soka ya Uingereza (EPL), iwapo United wataafikiana na klabu yake ya sasa PSG. Lakini itabidi Red Devils watoe kiasi kikubwa cha pesa kama fidia kwa mabwanyenye hao wa Ufaransa (Ligue 1), ili wavunje mkataba wa kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur.
Hayo yakijiri kwa upande mmoja, United wangali wanasaka mkufunzi atakayeshikilia mikoba hiyo kwa muda hadi ligi itakapotamatika Mei 22 mwaka ujao.Hata hivyo, makocha wengi wanaolengwa kwa kibarua hicho cha muda, akiwemo Laurent Blanc na Ralf Rangnick, tayari wana majukumu kwingineko.
Blank ni kocha wa Al Rangnick nchini Qatar, ambako msimu unaendelea hadi mwezi Machi. Rangnick ni mkurugenzi wa kiufundi wa klabu ya Lokomotiv Moscow nchini Russia – japo ligi itaenda likizo ya siku 10 Desemba.
Lucien Favre, 64, amekuwa bila kazi tangu atimuliwe na Borussia Dortmond ya Bundesliga kule Ujerumani mnamo 2020.Lakini kocha huyo amehusishwa na klabu nyingi za EPL ila akazikataa kazi hizo.
Pilkapilka za kusaka kocha atakayerithi mikoba ya Ole Gunnar Solskjaer ugani Old Trafford zinajiri wakati naibu mwenyekiti mkuu Ed Woodward akitarajiwa kuondoka mamlakani mwishoni mwa mwaka.
Licha yake kuanza kufunganya virago, klabu imesisitiza kwamba ndiye ataendesha shughuli hizo za kusajili mkufunzi mpya. Woodward na Meneja Mkurugenzi Richard Arnold ndio waliwasiliana na mwenyekiti mwenza Joel Glazer Jumamosi saa chache kabla ya kocha Ole Gunnar kufutwa kazi majuzi.
Woodward ndiye aliyetoa habari hizo mbaya kwa Solskjaer, na pia ndiye aliyemuuliza Carrick achukue jukumu la ukufunzi kwa muda.Kocha Muricio Potchettino amesema yuko tayari kuajiriwa na Manchester United iwapo watakubaliana na klabu yake ya PSG.
Lakini itabidi Manchester watoe kiasi kikubwa cha pesa kulipa PSG ili wavunje rasimi mkataba wa kocha huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur.
Next article
Polisi wakosa kunasa wezi wa benki Kisumu