Connect with us

General News

Jamaa, marafiki kiini cha masaibu ya wanariadha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jamaa, marafiki kiini cha masaibu ya wanariadha – Taifa Leo

Jamaa, marafiki kiini cha masaibu ya wanariadha

Na WAIKWA MAINA

RAIS wa Shirikisho la Riadha Kenya (AK) Jackson Tuwei amefichua kuwa mzigo wa kutegemewa na jamaa, rafiki na jamii pamoja na mivutano ya kurithi mali ndizo changamoto kubwa zinazokabili wanariadha wa Kenya.

Anasema kuwa changamoto hizo zinasababisha wanariadha kuwa na msongo wa akili kwa sababu kila jamaa anataka mgao wa tuzo wanashinda kutoka kwa mashindano ya kimataifa.Tuwei alikuwa akizungumza wakati wa duru ya tatu ya Mbio za Nyika za AK iliyofanyika katika eneo la Ol Kalou katika Kaunti ya Nyandarua wikendi iliyopita.

Duru hiyo ilivutia zaidi ya wanariadha 1,000, idadi hiyo ikiwa ni kubwa kuliko 800 waliojitokeza kwa makala yaliyopita. Baada ya Ol Kalou, mbio za nyika za AK zitaelekea eneo la Kapsokwony, Mount Elgon kaunti ya Bungoma wikendi hii.

Tuwei alisema kuwa wanariadha wanapowasili nchini kutoka mashindano ya kimataifa wanalakiwa na jamaa na rafiki ambao mara nyingi akili zao ziko kwenye kitita kilichopatikana badala ya kusherehekea mafanikio ya mwanariadha.

“Wanariadha wanaumia kimyakimya. Hawafurahii matunda ya kazi yao. Jamaa wanataka kusaidiwa kulipiwa karo na majukumu mengine. Makanisa pia yanawatumia mialiko chungu nzima ya harambee,” alieleza Tuwei.

Jamaa wengine hata wanataka kuhusishwa moja kwa moja katika kuendesha shughuli za kiuchumi za wanariadha. Wanatumia hata njia zisizofaa kusimamia mali na urithi. Wanariadha wetu wanaumia sana kutokana na ukatili huu,’ alieleza Tuwei.

Wakati huo huo, Tuwei ameshauri wanariadha kujiandaa kwa msimu ujao uliojaa mashindano yatakayoanza Januari 2022. AK imeandaa mashindano kadhaa yakiwemo ya Kaunti, kitaifa na kimataifa mwaka ujao.

Pia, alishauri vikosi vya usalama na vyuo vikuu viandae wanariadha wao kwa mashindano ya kitaifa yatakayofanyika katika Kaunti ya Uasin Gishu yatakayotangulia duru ya Mbio za Nyika Duniani katika kaunti hiyo.

Baada ya Ol Kalou, mbio za nyika za AK zitaelekea eneo la Kapsokwony, Mount Elgon kaunti ya Bungoma wikendi hii.