Connect with us

General News

Korir na Cheptonui kuongoza Wakenya 12 Malaga Marathon – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Korir na Cheptonui kuongoza Wakenya 12 Malaga Marathon – Taifa Leo

Korir na Cheptonui kuongoza Wakenya 12 Malaga Marathon

Na GEOFFREY ANENE

MARK Korir na Caroline Cheptonui wataongoza Wakenya 12 watakaowania mataji ya mbio za Zurich Malaga Marathon nchini Uhispania mnamo Desemba 12 asubuhi.

Solomon Kirwa, Timothy Kiplagat, David Barmasai, Raymond Kipchumba, Jopshat Kiprotich, Alice Jepkemboi, Beatrice Cheptoo, Pauline Mutwa na Jackline Atudonyang ni Wakenya wengine watakaotifua vumbi katika mbio za kilomita 42 ambazo zimevutia washiriki 4,000 mjini Malaga.

Washindi watatia mfukoni Sh383,527 kila mmoja na kuongezwa Sh127,842 wakivunja rekodi za Zurich Malaga Marathon zinazoshikiliwa na washindi wa 2019 Mkenya Martin Cheruiyot (saa 2:10:08) na Muethiopia Selamawit Getnet (2:27:56).

Marius Kitumai kutoka Bahrain ndiye mkimbiaji mwanamume aliye na muda bora kuliko washiriki wote wa kitengo hicho wa saa 2:05:47, sekunde 0.02 mbele ya Korir. Kwa upande wa kinadada, Cheptonui ana muda bora wa 2:22:34 dhidi ya Jepkemboi (2:28:14).

Watimkaji wengine 4,700 watashiriki mbio za kilomita 21 (Half Marathon). Mashindano haya hayakufanyika 2020 kwa sababu ya mkurupuko wa virusi vya corona.

Orodha ya washiriki mastaa

Wanaume

Marius Kitumai (Bahrain), saa 2:05:47

Mark Korir (Kenya) 2:05:49

Deribe Robi Melka (Ethiopia) 2:05:58

Solomon Kirwa (Kenya) 2:06:24

Limenih Getachew (Ethiopia) 2:06:47

Timothy Kiplagat (Kenya) 2:07:01

David Barmasai (Kenya) 2:07:18

Raymond Kipchumba (Kenya) 2:08:11

Kenneth Kiplagat (Kenya) 2:10:12

Nguse Amlosom (Eritrea) 2:10:15

Berhane Tsegay (Eritrea) 2:12:25

Jopshat Kiprotich (Kenya) marathon ya kwanza kabisa

Wanawake

Caroline Cheptonui (Kenya) 2:22:34

Alice Jepkemboi (Kenya) 2:28:14

Gadise Gudisa (Ethiopia) 2:30:30

Beatrice Cheptoo (Kenya) 2:33:06

Pauline Mutwa (Kenya) 2:41:32

Jackline Atudonyang (Kenya) marathon ya kwanza kabisa

Maritu Ketema (Ethiopia) marathon ya kwanza kabisa

Yeneabeba Maru Ejigu (Ethiopia) marathon ya kwanza kabisa

Tseginesh Mekonnin (Ethiopia) marathon ya kwanza kabisa

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending