Connect with us

General News

Raila atasalitiwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Raila atasalitiwa – Taifa Leo

Wandani wa Ruto: Raila atasalitiwa

CHARLES WASONGA na SHABAAN MAKOKHA

WANDANI wa Naibu Rais William Ruto wamedai kuwa kiongozi wa ODM Raila Odinga atasalitiwa na wale wanaunga mkono azma yake ya urais wakiwemo mabwanyenye wa Mlima Kenya.

Wanasiasa hao jana walisema dalili ya usaliti huo zilijitokeza Ijumaa katika uwanja wa Kasarani Ijumaa wakati wanasiasa wakuu nchini walikwepa mkutano wa Azimio la Umoja. Bw Odinga alitangaza rasmi azma yake ya kuwania urais kwa mara ya tano katika mkutano huo uliodhuhuriwa na wafuasi wake kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Lakini wakiongeza jana katika kaunti ya Turkana, Gavana wa kaunti hiyo Josephat Nanok, Stanly Kaptis (Baringo), Jackson Mandago (Uasin Gishu) walibashiri kuwa Odinga atasalitiwa tena katika safari yake ya kwenda Ikulu.

Wengine walioendeleza kauli hiyo ni wabunge Aden Duale (Garissa Mjini), Kimani Ichung’wa (Kikuyu) na James Lomenen (Turkana Kusini).“Wale ambao wamekuwa wakiendeleza ajenda yako sasa wanakutenga. Tafakari na upange upya siasa zako,” Bw Duale akamwambia Bw Odinga.

Mbunge huyo wa Garissa Mjini alisema kiongozi huyo anavuna alichopanda kwa sababu yeye pia alichangia kutengwa kwa Naibu Rais William Ruto alipoingia serikalini kupitia handisheki kati yake na Rais Uhuru Kenyatta.

Wanasiasa hao walikuwa wakiongea mjini Lodwar siku ya kufungwa kwa awamu ya sita ya sherehe ya kitamaduni kwa jina Tobong’u Lore.Hafla hiyo iliongozwa na Naibu Rais Dkt Ruto ambaye aliwasili katika kaunti ya Turkana Ijumaa baawda ya kufanya mkutano wa kisiasa kaunti ya Narok.

Vinara watatu wa muungano wa One Kenya Alliance (OKA) ni miongoni mwa viongozi ambao hawakuhudhuria mkutano wa Bw Odinga licha ya kualikwa. Wao ni Musalia Mudavadi (ANC), Kalonzo Musyoka (Wiper) na Moses Wetang’ula wa Ford Kenya.Mabwanyenye wa Mlima Kenya ambao juzi walimuidhinisha kama mgombeaji anayefaa kumrithi Rais Kenyatta, 2022 waliwakilishwa na mmiliki wa Shirika la Habari Royal Media Dkt SK Macharia.

Wakati huo huo, wabunge wa chama cha Amani National Congress (ANC) wamewapongeza vinara wa OKA kwa kukataa kuhudhuria mkutano wa Azimio la Umoja katika uwanja wa Kasarani, Nairobi, Ijumaa.Wakiongea katika mkutano wa kisiasa katika eneo bunge la Malava wakiongozwa na Seneta wa Kakamega wabunge hao walisema hatua hiyo ilionyesha kuwa muungano huo hautaunga mkono mgombeaji mwingine.

Wengine walioshikilia kauli hiyo ni Mbw Malulu Injendi (Malava) na Peter Nabulindo (Matungu)“Tunapongeza zaidi hatua ya Musalia Mudavadi, Moses Wetang’ula na Kalonzo Musyoka kukwepa mkutano wa Azimio la Umoja katika uwanja wa Kasarani.

Mudavadi ametangaza azma ya kuwania urais na hawezi kuhudhuria hafla ya kuidhinishwa kwa mshindani wake,” akasema Bw Malala. Bw Nabulindo alisema kuwa Mudavadi amethibitisha kuwa ni mgombeaji urais mwenye msimamo thabiti.

“Kitendo cha Mudavadi kimeondolea mbali uvumi unaoendelea mitandaoni kwamba huenda Mudavadi anamuunga mkono Bw Odinga,” akaeleza.Japo Mbw Mudavadi, Wetang’ula na Musyoka walikosa kufika katika mkutano huo licha ya kualikwa rasmi, vinara wenzao Gideon Moi na Cyrus Jirongo-UDP walihudhuria.

wa chama cha United Democratic Party (UDP) walihudhuria.Mkutano huo pia ulihudhuriwa na mawaziri sita wa serikali ya kitaifa, magavana 21, maseneto 30 na zaidi ya wabunge 80 wa vyama vya ODM na Jubilee.Bw Mudavadi, ambaye ametangaza nia ya kuwania urais, alisema kupitia twitter kwamba japo alialikwa rasmi, hangeweza kuhudhuria kutokana na shughuli za kibinafsi zilizombana“Raila Odinga ni mshindani wangu.

Japo nimealikwa sitahudhuria kwa sababu ya shughuli zingine ambazo nilikuwa nimeratibu awali. Namtakiwa kila la kheri kwa sababu kesho ni siku yake,” akasema.Awali, Bw Mudavadi alikerwa na hatua ya baadhi wa vinara wenzake kumwalika Bw Odinga katika hasla zao.

Kwa mfano, juzi kiongozi huo wa ANC alikasirishwa na hatua ya Bw Musyoka kumwalika Odinga katika mkutano wa wajumbe wa chama cha Wiper.Kiongozi huyo wa Wiper hata hivyo hakuhudhuria mkutano wa Azimio la Umoja, Kasarani kwa sababu alikwenda nchini Sudan Kusini kwa ziara rasmi.