Connect with us

General News

Siri kwa wakuzaji miparachichi Kenya kupata soko la avokado katika nchi za kigeni – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Siri kwa wakuzaji miparachichi Kenya kupata soko la avokado katika nchi za kigeni – Taifa Leo

Siri kwa wakuzaji miparachichi Kenya kupata soko la avokado katika nchi za kigeni

Na SAMMY WAWERU

MWAKA wa 2019 Kenya ilitia saini mkataba wa makubaliano na serikali ya Uchina, Kenya kuuza avokado nchini humo.

Hatua hiyo, ni fursa ya kipekee kisoko kwa wakulima wa humu nchini waliozamia uzalishaji wa maparachichi.

Taifa hili hufanya mauzo ya avokado kwa wingi Bara Uropa na nchi za Uarabuni.

Makubaliano ya Kenya na China yakitekelezwa kikamilifu, asilimia 40 ya mazao ya miparachichi yatakuwa yakiuzwa nchini humo.

Licha ya fursa hiyo, baadhi ya kampuni na mashirika yanayounganisha wakulima kwa masoko ya nchi za kigeni mazao wanayosambaza yamekosolewa kwa kutoafikia vigezo faafu.

Machi 2021, Mamlaka ya Kusimamia Kilimomseto iliondoa marufuku ya miezi minne Kenya kuuza avokado aina ya Hass na Fuerte katika masoko ya kigeni, baada ya kuthibitisha wakulima kuhitimu mahitaji ya ukomavu wa matunda haya.

Mabroka wanasemekana kuchangia marufuku hiyo, kwa kuuzia mashirika na kampuni matunda ambayo hayajakomaa.

Taasisi ya Mbegu na Ustawishaji wa Mimea (Kephis), ndiyo inasimamia uuzaji wa avokado katika masoko ya kigeni.

Nusu ya mapato ya matunda yanayouzwa nje ya nchi, hutoka kwa maparachichi.

Rangi nje ya maparachichi yaliyokomaa na kuvunwa. PICHA | SAMMY KIMATU

Huku soko la matunda haya ughaibuni likinoga, wakulima wanahimizwa kuzingatia ushauri kitaalamu na njia bora za kilimo.

“Wapande miche kutoka kwa wazalishaji walioidhinishwa na Kephis,” Laban Mwaura, mtaalamu na naibu meneja wa masuala ya mashauri shambani Kakuzi PLC ashauri.

Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Mimea na Uimarishaji Mifugo (Karlo), inaongoza katika uzalishaji wa miche bora.

Upanzi wa parachichi ukitegemea vipimo kitaalamu na muundo wa shamba, mdau huyu anahimiza wakulima kupanda miche kwa kutumia mchanganyiko wa mbolea, udongo wa juu, laimu na fatalaiza iliyosheheni Phosphorus.

Miche bora ni iliyoimarishwa, kwa njia ya kupandikiza (grafted).

Mwaura anasema, shimoni mkulima asiache nafasi kubwa juu ili miche isioze maji yanapokusanyika.

“Sitiri miche hadi ipate nguvu kujiendeleza kukua,” mtaalamu huyu aelekeza, akihimiza umuhimu wa maji, kuboresha miparachichi kwa mbolea na fatalaiza zenye virutubisho faafu, kupogoa, na pia kuwa mwangalifu kwa wadudu na magonjwa.

“Siri ya kilimo cha matunda ni kuwa na maji ya kutosha. Mkulima akumbatie mfumo wa kunyunyuzia mimea iliyo mashambani maji kwa kutumia mifereji,” asisitiza Daniel Mwenda, mtaalamu wa matunda na miti.

Chini ya vigezo bora kitaalamu, avokado zilizoimarishwa huanza kutunda miaka miwili na nusu hadi mitatu baada ya upanzi.

Kulingana na Mwaura, matunda yaliyokomaa vyema yanapaswa kuwa ya rangi ya kijani cheusi (dark green).

“Kiwango cha unyevuunyevu wa maji kiwe chini ya asilimia 77,” adokeza.

Kiwastani, mti uliotunzwa vyema una uwezo kuzalisha zaidi ya maparachichi 500 kwa mwaka.

Esther Nderi ni mkulima wa maparachichi Kaunti ya Murang’a na anaridhia ukuzaji wa matunda haya.

Afisa huyu mstaafu wa masuala ya mifugo, aliingilia ukulima wa avokado 2017, mwaka mmoja baada ya kustaafu.

“Niling’oa mikahawa yote na kupanda maparachichi,” anaiambia Taifa Leo, akikumbuka changamoto alizopitia katika kilimo cha kahawa.

Mkulima huyu wa eneo la Makuyu, ana zaidi ya miti 100 ya avokado za Hass anazokuza katika ekari moja.

Husambazia Kakuzi PLC, kampuni ambayo huuza matunda nje ya nchi. Wakulima wa mashamba madogo wanahimizwa kuwa kwenye miungano au vyama vya ushirika ili kuwaunganisha na soko bora.

Kenya imeorodheshwa nchi ya nane bora duniani katika ukuzaji wa maparachichi.

Kati ya Januari na Machi 2021, iliuza tani 26, 481 za matunda haya katika masoko ya kigeni, ikilinganishwa na tani 15, 101 kipindi kama hicho mwaka uliopita, 2020.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending