[ad_1]
Mahakama yamwachilia diwani aliyefungwa jela
Na MAUREEN ONGALA
MAHAKAMA ya Malindi Ijumaa ilimwachilia huru diwani wa Mkomani, Kaunti ya Lamu, Yahya Mohamed Shee aliyefungwa miaka tisa unusu kwa madai ya kuwasaidia washukiwa watatu wa dawa za kulevya kuhepa.
Katika uamuzi wake, Jaji Rueben Nyakundi alisema kuwa hakubaliani na uamuzi wa korti ya chini iliyomfunga diwani huyo kwa kuwa kulikuwa na masuala mengi katika kesi hiyo ambayo hayakujitokeza wazi wazi.
Alisema kuwa polisi walikosa kutoa taarifa kamili kuhuiana na kesi hiyo huku mashahidi wakikinzana katika ushahidi wao.
Kadhalika, alisema kuwa polisi walishindwa kutoa washukiwa wengine wanaodaiwa kuhusika katika kesi hiyo.
“Polisi hawakueleza ni kwa nini washukiwa hao hawakukamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani kama alivyofanyiwa diwani huyo. Nashangaa ni kwa nini polisi hao walishindwa kuwakamata wahalifu hao wengine. Hii si haki,” akasema hakimu Nyakundi.
[ad_2]
Source link