Connect with us

General News

Natembeya aonya wanasiasa kuhusu Mau – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Natembeya aonya wanasiasa kuhusu Mau – Taifa Leo

Natembeya aonya wanasiasa kuhusu Mau

Na GEORGE SAYAGIE

KAMISHNA wa Rift Valley George Natembeya amewaonya baadhi ya wanasiasa dhidi ya kutumia suala la uhifadhi wa Msitu wa Mau kwa manufaa yao ya kisiasa.

Bw Natembeya, ambaye alikuwa akizuru eneo la South Rift kukagua miradi inayofadhiliwa na serikali ya kitaifa, alisema suala hilo halifai kujadiliwa tena katika majukwaa ya kisiasa.Kamishna huyo alioenakana kurejelea kauli ya Naibu Rais William Ruto aliyotoa juzi kwamba ataendeleza uhifadhi wa msitu huo ikiwa atachaguliwa kuwa rais mwaka ujao.

“Wanasiasa wakome kabisa kurejesha suala la uhifadhi wa msitu wa Mau katika siasa za kusaka kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2022. Hili suala linashughulikiwa na serikali na wanasiasa wasilitumie kusaka kura kutoka kwa raia,” akasema Bw Natembeya.“Hawa watu wakome kutoa taswira mbovu kwamba shida inayokumba Msitu wa Mau inahusu jamii moja au nyingine.

Wale wanaodhani kwamba serikali itawaruhusu watu kurejea katika msitu wa Mau wanajidanganya,” akaongeza.Katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, Dkt Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi walivutana kuhusu suala la uhifadhi wa msitu huo.

Katika ziara yake katika eneo hilo majuma mawili yaliyopita, Seneta Moi aliapa kuwasaidia watu ambao walifurushwa kutoka msitu huo mnamo 2019.Mwenyekiti huyo wa Kanu alisema Dkt Ruto ndiye anapaswa kulaumiwa kwa madhila ambayo watu hao wanapitia kwa sababu alichelea kuwasaidia.

Akiwahutubia mamia ya watu katika kituo kimoja cha kibiashara eneo hili, Bw Moi aliahidi kuwa atamjuza Rais Uhuru Kenyatta matatizo yao.“Nitawaletea matokeo baada ya siku 12 nitakaporejea eneo hili tena.” Seneta Moi akasema.

Katika ziara yake katika kaunti ya Narok wiki jana, Dkt Ruto alipuuzilia mbali madai kuwa alipinga mpango wa uhifadhi wa msitu wa Mau.Alisema amekuwa mstari wa mbele katika kutetea uhifadhi wa misitu.“Ninaunga mkono uhifadhi wa Mau na misitu mingine nchini ambayo ni vianzo vya maji nchini.

Aidha, ninaunga mkono mpango wa upanzi wa miche ya miti katika msitu huo, unaoendeshwa na serikali ikiwemo uwekaji ua,” akaeleza.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending