Connect with us

General News

Wataalamu wa afya na sayansi barani Afrika watuzwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wataalamu wa afya na sayansi barani Afrika watuzwa – Taifa Leo

Wataalamu wa afya na sayansi barani Afrika watuzwa

NA PAULINE ONGAJI 

TANGU mkurupuko wa maradhi ya Covid-19, Afrika imeonyesha ubabe wake katika masuala ya utafiti wa kimatibabu.

Hili lilidhihirika katika kongamano la kwanza la kimataifa kuhusu afya ya umma (CPHIA 2021) juma lililopita ambapo kuna baadhi ya wataalam waliotuzwa kutokana na mchango wao katika sayansi, utafiti na ustawi wa Afrika.

Baadhi ya waliotuzwa katika hafla hiyo ni pamoja na Profesa Jean-Jacques Muyembe-Tamfum, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya utafiti wa kimatibabu, na profesa wa virolojia ya kimatibabu katika Chuo Kikuu cha Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Prof Muyembe aidha ni mshauri mkuu wa kamati ya kimataifa ya dharura za kiafya kuhusu maradhi ya Ebola katika WHO.

Prof Muyembe mmoja wa wataalam wa kikundi cha Yambuku Catholic Mission waliopeleleza mkurupuko wa kwanza wa Ebola, na kisha akafanya kazi katika kikundi cha WHO kilichotekeleza utambuzi na udhibiti wa maradhi haya wakati wa kwanza nchini DRC.

Prof Salim Abdool Karim. Picha/CPHIA

Mwingine aliyetuzwa ni Prof Salim Abdool Karim kutoka Afrika Kusini. Prof Abdool ni mtaalamu wa afya ya umma na elimu ya magonjwa ya mlipuko, na naibu mwenyekiti wa Baraza la kimataifa la kisayansi.

Aidha, mtaalamu huyu ni mkurugenzi wa CAPRISA, utafiti wa kwanza kuonyesha kwamba aina fulani ya jeli ingetumika kupunguza uwezekano wa mtu kuambukizwa virusi vya HIV.

Wengine waliotambuliwa ni pamoja na wenyekiti wenza wa CPHIA 2021, Prof Senait Fisseha, na Prof Agnes Binagwaho, kutokana na ufanisi wao katika uongozi wa masuala ya kiafya ulimwenguni.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending