Connect with us

General News

Viongozi zaidi, wazee wapinga mkutano wa Atwoli Ijumaa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Viongozi zaidi, wazee wapinga mkutano wa Atwoli Ijumaa – Taifa Leo

Viongozi zaidi, wazee wapinga mkutano wa Atwoli Ijumaa

Na SHABAN MAKOKHA

VIONGOZI katika eneo la magharibi wanaendelea kupinga mkutano ambao katibu mkuu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi (COTU) Francis Atwoli, ameitisha katika uwanja wa Bukhungu kutangaza mwelekeo wa kisiasa wa eneo la Magharibi.

Aliyekuwa Seneta wa Kakamega Boni Khalwale, Mbunge wa Nambale Sakwa Bunyasi, Alfred Agoi (Sabatia), Beatrice Adagala (Mbunge Mwakilishi wa Vihiga) na mwenyekiti wa ANC Kelvin Lunani wamemshutumu Bw Atwoli kwa kuyumbisha wapiga kura wa magharibi mwa Kenya ili kuafiki matakwa yake.

Bw Bunyasi alisema Katibu huyo Mkuu wa COTU hana mamlaka ya kuamua mwelekeo wa kisiasa wa jamii ya Waluhya.

“Akome kudhani kwamba atawaelekeza wapigakura katika kuamua yule watakayempigia kura na yule hawatampigia kura. Wapigakura wa eneo la magharibi wako na uwezo wa kujiamulia watakayempigia kura. Hawafai kutishwa,” akasema Bw Bunyasi.

Naye Dkt Khalwale alimtaka Bw Atwoli kukoma kutumia urafiki wake na baadhi ya viongozi wa magharibi kumpigia debe kiongozi wa ODM Raila Odinga.

“Hatumtaki Raila Odinga kuhudhuria mkutano wa watu wa jamii ya Waluhya. Tuko na viongozi wetu ambao wana uwezo wa kuongoza mikutano kama hiyo lakini wamewekwa kando huku Raila akipendelewa,” akalalamika.

Wanasiasa hao pia wanawataka maafisa wa usalama kuendesha shughuli zao kisheria na wakome kutumiwa kuwatisha watu wengine wanaopinga misimamo ya kisiasa ya watu fulani kutoka eneo hilo.

Jumanne asubuhi, makundi mawili kinzani yalikabiliana mjini Kakamega kuhusiana na mkutano huo maarufu kama, Bukhungu II.

Makabiliano hayo yalitokea wakati wazee wa Butsotso walikuwa wakiwahutubia wanahabari katika mkahawa wa Golden Inn, mjini Kakamega kupinga mkutano huo.

Hapo ndipo walivamiwa na vijana waliodaiwa kuwa wafuasi wa ODM na kuvuruga kikao hicho.