Connect with us

General News

Polisi anayedaiwa kuua mkubwawe kuzuiliwa siku 8 – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Polisi anayedaiwa kuua mkubwawe kuzuiliwa siku 8 – Taifa Leo

Polisi anayedaiwa kuua mkubwawe kuzuiliwa siku 8

Na MACHARIA MWANGI

AFISA wa polisi wa cheo cha koplo aliyemuua mkubwa wake kwa kumpiga risasi siku ya Krismasi atazuiliwa kwa siku nane uchunguzi kuhusu kisa hicho ukiendelea.

Afisa huyo, Joseph Kamau Muthunga aliyekamatwa mjini Nakuru baada ya kutekeleza kisa hicho Naivasha, alifikishwa mahakamani jana Jumanne ambapo polisi waliomba muda zaidi wakamilishe uchunguzi.

Bw Muthunga analaumiwa kwa kumuua Sajini mkuu Ayub Polo katika kambi ya polisi.

Inadaiwa kwamba mshukiwa alimpiga risasi mkubwa wake baada ya kutofautiana katika karamu ya Krisimasi.

Baada ya kutekeleza mauaji hayo, inasemekana alitoweka lakini akakamatwa akiwa mjini Nakuru akiendelea kuburundika na kupelekwa Naivasha alikofikishwa kortini jana Jumanne.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending