Connect with us

General News

Sokomoko bungeni ni dalili hatari uchaguzini – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Sokomoko bungeni ni dalili hatari uchaguzini – Taifa Leo

TAHARIRI: Sokomoko bungeni ni dalili hatari uchaguzini

Na MHARIRI

WASIWASI wa wadau katika sekta ya utalii kuhusu hali ya biashara zao wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi mkuu una mashiko ikizingatiwa matukio ya jana Jumatano katika bunge la kitaifa ambako ghasia kali zilitokea.

Wabunge ambao watakuwa wakishiriki kwenye kampeni hizo walizua vurugu na kupigana mbele ya kamera zilizopeperusha matukio moja kwa moja.

Ni hali ambayo wadau wa utalii wanahisi kwamba, ikiwa itatokea wakati wa kampeni na baada ya uchaguzi, huenda biashara zao zilizoathiriwa na janga la corona zikakosa kufufuka.

Hofu yao inatokana na tajiriba yao katika chaguzi za awali ambapo watalii huepuka Kenya kwa sababu ya ghasia. Kwa wadau katika sekta hiyo, hofu yao ni kuhusu biashara zao zinazochangia katika ukuaji wa uchumi huku kwa wabunge waliopigana bungeni, ni kulinda maslahi yao.

Ukuaji wa uchumi huwa unatagemea uthabiti wa kisiasa katika nchi yoyote ile ulimwenguni na kwa kweli, matukio ya jana katika bunge na malumbano ambayo wanasiasa wamekuwa wakiendeleza katika mikutano ya kisiasa hayatoi taswira nzuri kuhusu hali ya baadaye ya uchumi wa Kenya.

Sokomoko zilizotokea bungeni zinaweza kuchochea wafuasi wa mirengo ya kisiasa kuanza kuvurugana na kusababisha ghasia.

Ili kuepuka hali kama hiyo kutokea, wanasiasa wanafaa kuvumiliana, kuendesha kampeni zao kwa heshima na kudumisha uadilifu.

Watungaji wa sheria wanapokosa heshima baina yao, itakuwa vigumu kushawishi wawekezaji kwamba kuna mazingira bora ya kuendesha biashara nchini.

Sio tu wawekezaji katika sekta ya utalii bali ni wa sekta zote za uchumi.

Iwapo wanasiasa wanakosa kujidhibiti, itakuwa vigumu kushawishi wafanyabiashara ambao wamekuwa wakipata hasara kila baada ya miaka mitano kuwa kutakuwa na amani kipindi cha kampeni na baada ya uchaguzi wa mwaka ujao.

Hali kama hii ikitokea, na tunarudia kwamba yaliyotokea jana ni ishara za hali mbaya, uchumi utapata pigo kubwa ikizingatiwa uliathiriwa kwa kiwango kikubwa na janga la corona.

Kwa kweli abunge hawawezi kuhubiri amani na kuvumiliana ilhali wao wenyewe hawawezi kusikizana na kuelewana.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending