Connect with us

General News

Teknolojia ya trei kukuza miche – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Teknolojia ya trei kukuza miche – Taifa Leo

Mbinu za Ukulima: Teknolojia ya trei kukuza miche

Na SAMMY WAWERU

UFANISI katika kilimo unategemea mambo kadha wa kadha, kuanzia pembejeo, rutuba ya shamba, kuwepo kwa maji ya kutosha na kuzingatia vigezo faafu kitaalamu.

Ezekiel Kaberi ambaye ni mkulima wa mimea aina aina ya vyakula Kaunti ya Kiambu, anasema kabla ya kujitosa rasmi kwa shughuli za kilimo, alizingatia matakwa hayo.

Cha kwanza kufanya ni utafiti wa kina kujua siri kufanikisha malengo yake katika zaraa.

Utafiti huo unajumuisha, kiini cha maji ya kutosha kuendeleza kilimo na hatimaye akapata shamba lililoafikia hitaji la kiungo hicho muhimu.

“Nilipokuwa nikitafuta shamba, nilitilia maanani eneo lililo na maji ya kutosha,” asema.

Ni mkulima wa mazao mabichi ya shambani yenye thamani, kama vile; Bokoli, Koliflawa, celery, pilipili mboga za rangi tofauti na matango, kati ya mengineyo.

Wakati wa mahojiano, shambani mwake eneo la Riara Ridge, Limuru, Kaunti ya Kiambu, aliiambia Akilimali kwamba kiini chake cha maji, ni ya yanayochipuka ardhini, ambapo ameyateka kwa vidimbwi na visima.

“Nina jenereta kadhaa zinazotumia nguvu za umeme kuyapampu na kusambaza,” adokeza.

Amekumbatia mfumo wa kunyunyuzia mimea na mashamba maji kwa mifereji (Irrigation).

Ezekiel Kaberi amekumbatia matumizi ya mifereji kunyunyuzia mimea na mashamba maji kama inavyoonekana kwenye picha hii akiwa katika shamba lake lililoko eneo la Riara Ridge, Limuru, Kaunti ya Kiambu. PICHA | SAMMY WAWERU

Chini ya mfumo huo, yapo matumizi ya paipu zilizosindikwa kwenye mashine ya mimea kudondoa maji (drip) na mabomba ya kuzunguka (sprinkler).

Kulingana na mtaalamu wa kilimo Daniel Mwenda, siri ya kufanikisha shughuli za kilimo hususan matunda, mboga na viungo vya mapishi ni kuwepo na chanzo cha maji ya kutosha.

“Maji ndiyo nguzo kuu ya kilimo. Wakulima wakumbatie mfumo wa kunyunyizia mimea na mashamba maji kwa mifereji,” Mwenda ashauri.

Kaberi, mbali na kuhakikisha eneo alilopata lina maji ya kutosha, anasema alikuwa makini kutafiti kuhusu soko.

“Himizo kupanua mradi lilichochewa na wingi wa wateja niliopata. Tayari nilikuwa kwenye soko,” aelezea, akidokeza kwamba alikuwa amepata mianya mingi ya soko.

Ni msambazaji mkuu wa mazao mabichi ya shambani katika supamaketi, hoteli na maduka ya vyakula, Nairobi na Kiambu.

Kero ya pembejeo ambazo hazijaafikia ubora wa bidhaa, hasa mbegu, fatalaiza na pia dawa dhidi ya wadudu na magonjwa, hakukwepa.

Anasema kupata mbegu na miche bora, ilikuwa kibarua na ndiposa akahusisha Taasisi ya Mbegu na Ustawishaji wa Mimea (Kephis), kupata suluhu.

Ana kivungulio chenye ukubwa wa mita 8 kwa 13, anachotumia kuzalisha miche. Aidha, kinasitiri miche ipatayo 300, 000.

Akiwa miongoni mwa wakulima wa mashamba makubwa nchini, Kaberi anasema hatua ya kujikuzia miche inampunguzia gharama kwa kiwango kikuu.

“Kila wiki, huhamisha miche 10, 000 kwa minajili ya upanzi,” asema.

“Huokoa Sh30, 000 kila wiki kwa kujizalishia,” anaongeza.

Huku wanasayansi na wataalamu wakihimiza haja ya kukumbatia mifumo ya Sayansi na Teknolojia ya kisasa, kama vile Bayoteknolojia, kuboresha kilimo, Kaberi hutumia trei kukuza miche.

“Trei zinafanikisha kati ya asilimia 95 – 100 mbegu kuota na kuchipuka kuwa miche,” asema.

Ni mfumo wa kisasa, wenye manufaa tele ukilinganishwa na tuta au kitalu cha udongo katika eneo tambarare.

“Eneo tambarare asilimia 60 – 70 pekee ndiyo hufanikiwa,” anasema.

Isitoshe, mfumo wa trei miche inakua salama chini ya matunzo ya kivungulio, ambapo athari za wadudu na magonjwa hudhibitiwa.

Ezekiel Kaberi akielezea kuhusu teknolojia ya trei kukuza miche shambani mwake eneo la Riara Ridge, Limuru, Kaunti ya Kiambu. PICHA | SAMMY WAWERU

Badala ya kununua mbegu za brokoli, huachilia baadhi ya mboga hizo zikomae ili apate mbegu kuzalisha miche.

Yote tisa, kumi Kaberi anajaribu kadri awezavyo kuhakikisha anaafikia vigezo vya kilimohai.

Anadokeza, hutumia mbolea ya mifugo hasa kinyesi cha mbuzi na kuku kufanya upanzi.

Kudhibiti asidi udongoni, huweka laimu ya kilimo.

Kabla kuingilia shughuli za kilimo, unahimizwa kufanya kipimo cha udongo ili kubaini kiwango cha asidi na laimu (pH) na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo cha Mimea na Uimarishaji Mifugo (Kalro) hutoa huduma hizo katika maabara yake kwa bei nafuu.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending