Connect with us

General News

Wazazi wasiharakishwe jinsi alivyoagiza Magoha – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Wazazi wasiharakishwe jinsi alivyoagiza Magoha – Taifa Leo

WANTO WARUI: Wazazi wasiharakishwe jinsi alivyoagiza Magoha

Na WANTO WARUI

Juma lililopita Waziri wa Elimu Prof George Magoha alitoa agizo kwa wakuu wa shule za sekondari kutowafukuza wanafunzi kwa kutolipa karo ya shule na badala yake wazazi waweke makubaliano na shule jinsi watakavyolipa pesa hizo.

Agizo hilo la waziri linatokana na kile alichokiita hali ngumu ya kiuchumi kwa wazazi wakati huu ambapo ulimwengu unapigana na gonjwa sugu la Covid-19.

Kulingana na waziri huyo, kuna wazazi wengi ambao hawataweza kupata pesa za kulipia karo kwani hali si nzuri. Hata hivyo, kunao watu wengi ambao wanajikimu vyema na biashara zao ziko imara au wanapata mishahara yao pasipo tatizo.

Agizo hilo la waziri linaweza kutumiwa na watu kama hawa katika kuwachezea walimu wakuu mchezo wa paka na panya.Inafaa ikumbukwe kuwa shule ni taasisi zinazoongozwa kwa bajeti ambazo hutegemea malipo ya karo.

Wanafunzi wa wa bweni, kwa mfano, huhitaji kula, kuoga, umeme na mambo mengine yasiyowezekana bila pesa. Ikiwa idadi kubwa ya wazazi haitaweza kulipa karo ya shule kwa muda ufaao, basi mipango mingi ya shule na masomo yanaweza kulemazwa na jambo hilo.

Mbali na kuzingatia agizo la Waziri, walimu wakuu wanafaa kukubaliwa kuchukua mwelekeo ufaao wa maamuzi ya malipo ya karo katika shule zao hasa wanapokabiliana na baadhi ya wazazi wasiopenda kulipa karo.

Mzazi ambaye anamrudisha mwanafunzi shuleni bila hata senti katika shule ya malazi anategemea mtoto wake alishwe kwa nini?

Mwafaka mzuri wa maelewano baina ya shule na mzazi unapovunjwa na mzazi kwa kutotimiza makubaliano ya mwafaka huo, basi ni muhimu mwalimu mkuu amtume mwanafunzi nyumbani alete karo.

Wakati mwingine walimu wakuu hupitia hali ngumu hasa serikali inapochelewesha kutuma pesa shuleni huku wazazi hawajalipa.

Kwa upande mwingine, kunao walimu wakuu ambao huongezea ada za ziada kama sehemu ya malipo ya shule huku wakisingizia ujenzi wa mabweni, madarasa, ununuzi wa mabasi na mengineyo. Ada kama hizi za ziada hazifai kufukuziwa mwanafunzi. kamwe.

Aidha kuna ukora mwingi ambao huendelea katika baadhi ya shule ambapo kwa mfano unakuta kuwa kwa muda wa miaka kumi au zaidi wanafunzi wamekuwa wakilipa ada za kununulia basi ambalo hata halipo.

Ni vizuri kila mzazi kuwajibikia majukumu yake katika malezi na masomo ya mwanawe. Suala la elimu ya mtoto ni jukumu la mzazi huku akisaidiwa na serikali lakini mzazi asikose kutekeleza jukumu lake la kulipa karo kwa kusingizia hali ngumu ya kiuchumi au kujificha katika kivuli cha agizo la waziri wa elimu.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Trending