[ad_1]
Jinsi ya kurudisha maji mwilini baada ya tizi
NA MWANDISHI WETU
Ni muhimu kuhifadhi maji mwilini mwako hata unapofanya mazoezi. Lakini kwa watu wengi ni ngumu kwao kuafikia azimio hili kwani hawapendi kunywa maji kabla, wakati na baada ya mazoezi.
Kwa hivyo mbinu hizi zitakusaidia kudumisha au kurejesha maji mwilini wakati na baada ya mazoezi:
Kula vyakula vilivyo na maji: Vyakula hivi ni kama vile supu na mtindi. Kadhalika kuna mboga kama vile kabeji, pilipili tamu au spinachi ambazo zaweza kusaidia kudumisha uowevu mwilini.
Kula tikiti maji: Kulingana na wataalamu, tunda hili linajumuisha asilimia 92 ya maji. Kadhalika tunda hili lina kiwango cha juu cha madini ya chumvi, calcium na magnesium suala linalolifanya kufaa katika harakati za kurejesha maji mwilini.
Tango: Tango ni aina ya mboga inayofahamika kwa utulivu wake. Kulingana na wataalamu mboga hii ina asilimia 96 ya maji na haina mafuta au kolesteroli iliyoganda, mbali na kuwa na kiwango cha juu cha vitamini K, vitamini B6 na madini ya chuma.
Stroberi: Mbali na kuwa na ladha tamu, tunda hili linajumuisha asilimia?92 ya maji. Pia lina kiwango cha juu cha nyuzi na vitamini C.
Maziwa ya kiwango cha chini cha mafuta: Maziwa huwa na kiwango cha juu cha madini ya calcium ambayo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mifupa yako inakuwa thabiti. Utafiti zaidi pia unaonyesha kuwa maziwa ni bora kwako zaidi ya maji na vinywaji vingine vya spoti wakati wa zoezi.
Maji ya nazi: Maji ya nazi ina viwango vya chini vya kabohaidreti mbali na asilimia kubwa ya madini ya potassium, suala linalofanya kinywaji hiki kuwa mwafaka wakati wa kufanya mazoezi.
[ad_2]
Source link