[ad_1]
ANC yasema haitishwi na Savula kujiunga na Azimio la Umoja
Benson Amadala Na Shaban Makokha
CHAMA cha Amani National Congress (ANC) kimesema kwamba hatua ya mbunge wa Lugari, Ayub Savula na mwenzake wa Teso Kaskazini, Oku Kaunya ya kuhama chama hicho wakati wa mkutano wa Azimio la Umoja kikisema haiwezi kukitikisa.
Katibu wa tawi la Kaunti ya Kakamega la chama hicho Prof Amukoa Anangwe alisema kuhama kwa wawili hao Ijumaa katika uwanja wa Bukungu mbele ya kiongozi wa chama cha ODM, Raila Odinga, hakushtui ANC.
“Baada ya mashauriano, tumeamua kwamba kuhama kwao sio tishio kwa chama na kwamba hatuwahitaji,” alisema Prof Anangwe.
Alimlaumu katibu wa muungano wa vyama vya wafanyakazi, Francis Atwoli na Gavana wa Kakamega, Wycliffe Oparanya kwa kupanga njama ya kuhujumu kiongozi wa ANC, Musalia Mudavadi kisiasa.
Chama hicho kimesema kwamba Bw Savula hakuwa naibu kiongozi wake alivyodai.Mwenyekiti wa ANC, Bw Kelvin Lunani alisema chama kitajaza nafasi ya naibu mwenyekiti kwenye mkutano wa kitaifa wa wajumbe utakaofanyika Januari 20.
“Nafasi ambayo mbunge wa Lugari anadai anashikilia imekuwa tupu kwa miaka mingi. Kama ANC, hatuna naibu kiongozi wa chama licha ya mbunge Ayub Savula kuzunguka akidai anashikilia nafasi hiyo,” alisema Bw Lunani.
Bw Savula anatarajiwa kupigwa vita na ANC baada ya kumtema Bw Mudavadi ili ashirikiane na Bw Odinga.“Kamati ya Kitaifa ya Usimamizi ya chama chetu, inatayarisha NDC na pia kuweka ajenda kabla ya Januari 20 2022,” alisema.
Bw Lunani. Wakati huo huo imeibuka kuwa ushindani wa tiketi ya ANC kugombea ugavana kaunti ya Kakamega kati ya Bw Savula na seneta wa kaunti hiyo Cleopas Malala, huenda ilichangia kuhama kwa mbunge huyo wa Lugari.
[ad_2]
Source link