Connect with us

General News

Kanuni mpya zatoa afueni kwa waliochukua mikopo ya simu – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kanuni mpya zatoa afueni kwa waliochukua mikopo ya simu – Taifa Leo

Kanuni mpya zatoa afueni kwa waliochukua mikopo ya simu

Na WANDERI KAMAU

KAMPUNI za kuwakopesha watu pesa kwa njia ya mtandao zitazuiwa kuwaweka wateja walioshindwa kulipa mikopo ya chini ya Sh1,000 kwa Mamlaka ya Kudhibiti Watu Waliovunja Masharti ya Mikopo (CRB) kuanzia Machi.

Kulingana na Kanuni Mpya za Kudhibiti Utoaji Mikopo kwa Mitandao 2021, kampuni hizo zitaruhusiwa tu kuwasilisha majina ya watu waliovunja kanuni za kulipa mikopo ya zaidi ya Sh1,000.

Ikitoa kanuni hizo mpya, Benki Kuu ya Kenya (CBK), inasema hatua hiyo inalenga kuwalinda mamilioni ya Wakenya dhidi ya kuwekwa kwenye orodha hiyo kwa kushindwa kulipa kiwango kidogo cha pesa.

Benki ilisema kampuni zitakazokiuka masharti hayo mapya zitakuwa kwenye hatari ya kunyang’anywa leseni zao au kutozwa faini kali.

Masharti hayo ni sehemu ya mabadiliko yaliyofanyiwa sheria inayoipa benki hiyo mamlaka kuamua kiwango cha riba ambacho kampuni zitakuwa zikiwatoza wateja wake kwa mikopo wanayochukua.

Hilo linalenga kulainisha riba zinazotozwa na kampuni hizo kwa kubuni mwongozo sawa wa kifedha kama ule unaozingatiwa na benki za kawaida.

“Itakuwa hatia kwa kampuni yoyote ya kutoa mikopo kwa njia ya mtandao kuwasilisha jina la mteja au mtu yeyote aliyeshindwa kulipa mkopo wa chini ya Sh1,000 kwa CRB ili kuadhibiwa,” yanaeleza mapendekezo hayo.

Kanuni hizo zinaendelea kutathminiwa kwa kina kabla ya kuchapishwa katika gazeti rasmi la serikali Machi 23, 2022, wakati CBK itaanza kuzitekeleza.

Baadhi ya kampuni za kutoa mikopo zimekuwa zikilaumiwa kwa kuwatoza wateja riba za juu kuliko viwango vilivyowekwa.

Takwimu kutoka CBK zinaonyesha kuwa kati ya watu 4.6 milioni waliowasilishwa kwa CRB kwa kukiuka masharti ya ulipaji mikopo, wengi ni wale walioshindwa kulipa chini ya Sh1,000.

Kati ya mwezi Aprili na Desemba 2020, serikali ilizizuia kampuni hizo kwa muda kuwasilisha majina ya watu hao kwa mamlaka hiyo, kama njia ya kuwalinda Wakenya kutoka kwa athari za janga la virusi vya corona.

Septemba mwaka uliopita, Rais Uhuru Kenyatta aliziagiza taasisi za kifedha kutowasilisha majina ya watu waliochukua mikopo ya chini ya Sh5 milioni kwa CRB kwa mwaka mmoja, hadi hali kiuchumi iimarike nchini.