[ad_1]
Wafanyakazi wamshinikiza Gavana ajiuzulu
Na RUTH MBULA
MAMIA ya wafanyakazi walioshushwa vyeo katika Kaunti ya Nyamira wanaendeleza vita vya kumwondoa uongozini gavana wa kaunti hiyo Amos Nyaribo.
Wafanyakazi hao walisema kuwa kumwondoa uongozini gavana huyo kutafanya wapandishwe vyeo kwani ndiye kizuizi.
Wakizungumza na wanahabari, walisema kuwa serikali ya kaunti hiyo ilikosa kutimiza amri ya korti ya ajira ya kuwapandisha vyeo wafanyakazi zaidi ya 1,000.
Badala yake, serikali ya kaunti hiyo imekubali maombi ya walalamishi wanne wakuu pekee waliowasilisha kesi ya kupinga hatua hiyo kortini.
Wanne hao ni mkurugenzi wa ushiriki wa umma, Dan Onyancha, meneja wa malipo, Lewis Oburu, mkurugenzi wa idara ya usimamizi wa utumishi wa umma, Douglas Osoro na afisa wa mipango katika kaunti hiyo, Lamech Machuki.
Hata hivyo, hatua hiyo imewafanya baadhi ya wafanyakazi kumshutumu msimamizi wa malipo, Bw Oburu na hata kumtaka gavana Nyaribo kujiuzulu.
Next article
TUSIJE TUKASAHAU: Miradi ya serikali yafaa kukamilishwa
[ad_2]
Source link