Connect with us

General News

Kitendawili kuhusu idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na selimundu magharibi mwa Kenya – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Kitendawili kuhusu idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na selimundu magharibi mwa Kenya – Taifa Leo

Kitendawili kuhusu idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na selimundu magharibi mwa Kenya

NA MWANDISHI WETU

Uwezekano wa mtoto kuzaliwa na ugonjwa wa selimundu (sickle cell) katika maeneo ya magharibi mwa Kenya ni mkubwa ikilinganishwa na maeneo mengineyo ya nchi.

Ugonjwa wa selimundu unatokana na dosari ya seli nyekundu za damu. Seli nyekundu hushindwa kusafirisha oksijeni mwilini hivyo kumfanya mwathiriwa kuhisi maumivu makali yasiyo na kifani.

Takwimu za wizara ya Afya zinaonyesha kuwa asilimia 18 ya watoto katika maeneo ya Nyanza na Magharibi huzaliwa na chembechembe zinazosababisha ugonjwa wa selimundu.

Kati ya watoto wanaozaliwa na chembechembe hizo, asilimia 4.5 hupatwa na maradhi hayo.Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), mtu anaweza kuzaliwa na chembechembe za ugonjwa huo lakini asiugue.

Mtu anaweza kubeba chenbe za ugonjwa huo bila kujua na kuzipitisha kwa mwanawe au mjukuu wake.

Takwimu za wizara ya Afya zinaonyesha kuwa ukanda wa Pwani unafuatia kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa na chembechembe zinazosababisha ugonjwa wa selimundu.

Watoto 6,000 huzaliwa na tatizo la selimundu kila mwaka nchini Kenya, kulingana na Wizara ya Afya.

Lakini kati ya asilimia 50 na 80 ya watoto wanaozaliwa na tatizo hilo hufariki kabla ya kufikisha umri wa miaka mitano.

Wengi wa watoto hufariki kwa sababu wazazi hawana ufahamu wa kutosha kuhusiana na maradhi ya selimundu hivyo hawachukui hatua za haraka kuwatafutia matibabu.