[ad_1]
Samaki, mazao kusafirishwa kwa ndege kutoka Uwanja wa Kisumu
WAVUVI na wakulima katika maeneo ya magharibi mwa Kenya huenda wakanufaika pakubwa baada ya serikali kutangaza mpango wa kuanza kusafirisha samaki na mazao ya kilimo kwa ndege kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kisumu (KIA).
Kulingana na mwenyekiti wa Shirika la Maendeleo katika Ukanda wa Ziwani – Kisumu (KLDC) Edward Ouko, ndege ya kwanza ya kubeba mazao na samaki itaanza safari Januari 8, mwaka huu.
Hiyo ni baada ya wawekezaji kukamilisha ujenzi wa eneo ambapo samaki na mazao ya kilimo yatahifadhiwa uwanjani hapo kabla ya kusafirishwa kwa ndege.
[ad_2]
Source link