Connect with us

General News

Uhuru aenjoi Wakenya kuhusu stima – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Uhuru aenjoi Wakenya kuhusu stima – Taifa Leo

Uhuru aenjoi Wakenya kuhusu stima

Na LEONARD ONYANGO

WAKENYA wataendelea kuumia kwa kulipa gharama ya juu ya umeme huku Rais Uhuru Kenyatta akikwepa kutekeleza ahadi ambazo amekuwa akitoa tangu 2018 kuhusu punguzo la bei ya kawi.

Rais Kenyatta alikosa kutekeleza ahadi aliyotoa Oktoba 20, ambapo aliahidi kuwa bei ya umeme ingepunguzwa kwa asilimia 15 kufikia Disemba 24, mwaka jana.

Awamu ya pili ya punguzo la asilimia 15 ya gharama ya umeme ilifaa kutekelezwa kuanzia Machi mwaka huu.

“Wizara ya kawi, itahakikisha kuwa inatekeleza kikamilifu ripoti ya jopokazi lililoteuliwa kutathmini mikataba ya ununuzi wa umeme. Bei ya umeme itapungua kufikia Disemba 24.

“Kwa hivyo, Wakenya watasherehekea Krismasi bila mzigo wa ‘bili’ kubwa ya umeme,” alisema katika Sherehe za Mashujaa uwanjani Wanguru, Kaunti ya Kirinyaga.

Baadaye, kampuni ya kusambaza umeme, Kenya Power, iliahidi Wakenya kwamba ingetekeleza kikamilifu agizo hilo la Rais Kenyatta kwa kuwapunguzia Wakenya mzigo wa bei ya juu ya umeme. Kufikia sasa ahadi hiyo imesalia ‘hewa’.

“Kenya Power inawafahamisha kuwa awamu ya kwanza ya punguzo la bei ya umeme kwa asilimia 15 itatekelezwa Disemba 2021,” ilisema taarifa ya Kenya Power.

Kinaya ni kwamba, huku Wakenya wakiendelea kungoja kuanza kufurahia punguzo hilo, Mamlaka ya Mafuta na Kawi (Epra) tayari imechapisha bei mpya ya umeme ambapo raia watalazimika kulipa zaidi. Epra imeongeza ushuru wa bei ya mafuta kwa Sh0.42 hadi Sh4.63 kwa kilowati moja.

Katika hotuba yake ya kukaribisha Mwaka Mpya wa 2022, Rais Kenyatta alionekana kukwepa kuzungumzia punguzo la bei ya umeme kabla ya sherehe ya Krismasi na badala yake akasema: “Bei ya umeme itaendelea kupunguzwa zaidi kufikia robo ya kwanza ya mwaka wa 2022.”

Kauli hiyo ya Rais Kenyatta katika ujumbe wake wa Mwaka Mpya, ilifasiriwa na wataalamu kuwa punguzo hilo litaanza kutekelezwa Machi.

Oktoba 2018, Rais Uhuru Kenyatta alipokuwa akizungumza katika Chuo Kikuu cha Strathmore, aliagiza Waziri wa Kawi wakati huo, Bw Charles Keter, kupunguza bei ya umeme ndani ya mwezi mmoja.

“Lazima tushughulikie mambo ya stima, bei ya stima kwa ukweli kwa wenzetu wengi imepanda. Na leo hii ninaamrisha Waziri ndani ya mwezi mmoja apunguze bei ya stima ndio wananchi waweze kufanya biashara,” alisema Rais Kenyatta.

Kenya ni kati ya mataifa manne barani Afrika ambapo wananchi wanaumia zaidi kwa kulipa gharama ya juu ya umeme.

Ripoti iliyotolewa Septemba, mwaka jana, na kampuni ya Globalpetrolprices, ambayo hutathmini bei ya petroli na umeme katika mataifa mbalimbali duniani, ilibaini kuwa Wakenya wanalipa Sh24 kwa kila kilowati moja ya umeme.

Wastani kimataifa ni Sh15.Bei ya juu ya umeme nchini inachangiwa na mrundiko wa ushuru ambao hugeuka mzigo kwa watumiaji wa umeme.

Miongoni mwa ushuru uliojumuishwa katika bei ya stima nchini ni ushuru wa Thamani (VAT) wa asilimia 16, ada ya ubadilishanaji sarafu za kigeni, ada ya Epra kati ya matozo mengine.

Ukinunua umeme wa Sh100, kwa mfano, Sh48 hutumika kulipa ushuru; Sh13 huwa VAT, Sh24 huenda kwa Ushuru wa Kawi ya Mafuta, ubadilishaji wa sarafu ya kigeni hula Sh3.86 kati ya aina nyinginezo za ushuru. Mteja anayelipa Sh100 kihalisia hutumiwa umeme wa Sh52.

Machi mwaka jana, Rais aliteua jopokazi lililolenga kutathmini mikataba ya mauzo ya umeme baina ya kampuni ya Kenya Power na kampuni za kuzalisha kawi.

Katika ripoti yake, jopokazi hilo lilibaini kuwa Kenya Power iliafiki kununua kiasi kikubwa cha umeme usiotumika.

Jopokazi lilipendekeza kufutiliwa mbali baadhi ya mikataba ambayo imekuwa ikiumiza Wakenya kwa kulipia fedha nyingi bila umeme kuwafaidi.

Jopokazi hilo lililoongozwa na Bw John Ngumi lilisema kuwa kuvunjiliwa mbali kwa mikataba hiyo kutasaidia bei ya umeme kupungua kwa Sh8 kwa kila kilowati.

[ad_2]

Source link

Comments

comments

Facebook

Trending