Connect with us

General News

Jaji aonya serikali isilazimishe watu kuchanjwa – Taifa Leo

Published

on

[ad_1]

Jaji aonya serikali isilazimishe watu kuchanjwa – Taifa Leo

Jaji aonya serikali isilazimishe watu kuchanjwa

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA KUU jana ilisema kwamba agizo la kuizuia serikali kuwalazimisha wananchi kuonyesha cheti cha kupata chanjo ya Covid-19 lingali lipo ilhali wananchi wananyimwa huduma muhimu.

Wakati huo huo, Jaji Antony Mrima alikataa kuamuru Waziri wa Afya, Bw Mutahi Kagwe ashtakiwe kwa kukaidi na kudharau agizo la kusitisha amri yake kuhusu cheti cha cha kupokea chanjo hiyo.

Jaji Mrima alifahamishwa na wakili Harrison Kinyanjui kuwa Bw Kagwe alikaidi agizo la mahakama kwa kumwamuru naibu wake Dkt Mercy Mwangangi aagize wananchi wasio na cheti hicho wanyimwe huduma. Bw Kinyanjui alisema baadhi ya wananchi wamenyimwa huduma katika maduka ya makuu.

“Ninaomba hii mahakama imchukulie hatua kali waziri wa afya kwa kukaidi na kudharau agizo iliyositisha amri wananchi waonyeshe ushahidi wamepokea chanjo ya Covid-19,” Bw Kinyanjui alimrai Jaji Mrima.

Jaji Mrima hakuzugumzia suala hilo ila aliamuru kesi tano zinazopinga agizo hilo la Serikali ziunganishwe. na kusikizwa Feburuari 1 2022.

Bw Kinyanjui alimweleza Jaji Mrima baadhi ya wananchi walinyimwa huduma katika maduka ya Supa walipokosa kuonyesha ushahidi wa kupokea Covid-19.

Agizo la kusitisha agizo hilo la wananchi kunyimwa huduma ilitolewa Desemba 14, 2021 na Jaji Mrima.